Mzazi wa Barka Aeleza Kuhusu Mwanaye Kwenda Uholanzi

Mzazi wa Barka Seif amefunguka mengi baada ya kijana wake kupata nafasi ya kwenda kufanya majaribio kwenye timu za mpira wa miguu za watoto kwa muda wa wiki mbili ndani ya kituo maarufu duniani cha Ajax Amserdam Academy kilichopo nchini Uholanzi.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka (7) alitua kwenye kituo hicho kilichopo nchini Uholanzi Agosti 28, 2021 na tayari ameanza rasmi mazoezi ya pamoja na vijana wengine kwa ajili ya kufanyiwa majaribio kwenye timu za mpira wa miguu za watoto lengo kubwa likiwa ni kuwajenga zaidi katika soka.

Mzazi wa kiume wa Barka alisema kuwa kutokana namna ambavyo amekuwa akiona kijana wake akijituma katika kufanyia kazi mafunzo yote aliyokuwa akipatiwa akiwa nchini Tanzania kwenye kituo cha Magnet alipokuwa akijifunza mafunzo hayo ya mchezo wa mpira wa miguu.

Alisema kuwa anaamini kuwa kijana wake atafanya vizuri kwenye majaribio hayo na kwamba nafasi hiyo aliyoipata Barka inaweza kuwa ni sehemu ya kipekee katika kufanikisha kupeleka mbele na kutangaza nchi yetu kwenye mpira wa miguu.

Hata hivyo, alishukuru Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ushirikiano mkubwa ambao imekuwa ikimpatia kijana wake katika kumsapoti kipaji chake cha kusakata kabumbu bila kujali umri wake.

Barka anaandika historia ya nchi yetu Tanzania kutoa kijana mdogo kwenda kujiunga na moja kati ya vituo vikubwa vya soka dunianiĀ  na endapo atafanikiwa kufuzu na kuteuliwa kujiunga kwenye kituo hicho hivyo kuzidi kuitangaza vyema nchi pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kisoka hasa kimataifa zaidi.