Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Yatangaza Uchaguzi Mkuu

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza rasmi kufanyika kwa uchauguzi wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) utakao fanyika Novemba 27 mwaka huu mkoani Kigoma.

Tangazo kuhusu kufanyika kwa uchaguzi huo lilitolea Oktoba 09 na Makumu Mwenyekiti wa kama hiyo Wakili Benjamin Kalume alipokuwa mbele ya waandishi wa habari za michezo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Makao Makuu ya TFF.

Wakili Benjamin alieleza kuwa kwa mujibu wa katiba ya TPLB kifungu cha tisa (09) cha Kanuni za uchaguzi kinaeleza kuwa ukomo wa uongozi kwenye nafasi zinazotangazwa ni miaka 4, ambayo inakwisha mwaka huu hivyo kuwataka kufanya uchaguzi kama Katiba inavyotaka ambapo TFF imekasimiwa jukumu la kusimamia uchaguzi huo wa Bodi ya Ligi Tanzania kwa mijuba wa Katiba.

Akieleza kuhusu nafasi zinazogombewa, kalenda na taratibu za uchaguzi huo, Wakili Benjamin Kalume alisema nafasi hizo ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi nafasi moja (1), Makumu Mwenhyekiti nafasi moja(1), wawakilishi kutoka vilabu vya Ligi Kuu nafasi tatu(3) huku upande wa wawakilishi kutoka ligi daraja la Kwanza (kwa sasa Championship) na fasi moja (1) na wawakilishi kutoka vilabu ligi daraja la pili (First League) nafasi moja (1).

Aidha, Makamu Mwenyikiti wa kamati hiyo ya uchuguzi ya TFF, alifafanua kuhusu gharama za kuchukua fomu hizo akitanabaisha kuwa; fomu ya Mwenyekiti na Makamu itakuwa ni shilinigi laki mbili (200,000) ya Kitanzania huku nafasi ya ujumbe gharama zikitajwa kuwa kiasi cha shilingi laki moja (100,000) ya Kitanzania. Pesa hizo zitalipwa kwenye akaunti ya CRDB ya TFF, namba; 0150237315000.

Akitoa taarifa kuhusu kalenda ya uchaguzi Wakili Benjamin alisema kuwa uchukuaji wa fomu utaanza rasmi tarehe 11-15 Oktoba, 2021 ambapo fomu hizo zitapatikana TFF na kwenye tovuti ya TFF pia. Aliongeza kwa kutoa utaratibu mzima wa uchaguzi huo huku akiweka bayana kalenda ya matukio yote ya uchaguzi.

Alieleza kuwa baada ya zoezi la kurudisha fomu matokeo mengine yatakuwa hivi; Oktoba16-17, 2021 kikao cha mchujo wa wagombea; tarehe 18-19/10/2021 zoezi la kuchapisha na kubandika orodha ya awali ya wagombea. Mnamo tarehe 20-22/10/2021 zoezi la upokeaji na uwekaji wa pingamizi; tarehe 23-25/10/2021 kusikiliza mapingamizi hayo.

Matokeo mengine ni kwamba mnamo tarehe 26-28/10/2021 kutakuwa na zoezi la usaili wa wagombea; Tarehe 29-30/10/2021 Kutangaza na kubandika matokeo ya awali ya usaili wa wagombea; tarehe 31/10-02-11/2021 Sekretarieti kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye kamati ya maadili; mnamo tarehe 03-05/11/2021 kupokea kusikiliza na kutolea uamuzi masuala ya kimaadili; tarehe 06-07/11/2021 kutangaza matokeo ya kamati ya maadili; tarehe 08-10/11/2021 kipindi cha kukata rufani kwa wagombea; ambapo rufani hizo zitasikilizwa tarehe 11-13/11/2021 na kamati husika.

Mbali na matukio tajwa, matukio ya kukamilisha zoezi hilo la uchaguzi yatahusisha utoaji wa uamuzi wa rufani zoezi hili litafanyika 14/11/2021 na tarehe 15 -16/11/2021 kipindi cha kukata rufani dhidi ya kamati ya maadili; mnamo tarehe17-19/11/2021 kutakuwa na suala la kusikiliza rufani zoezi litakalo fanywa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF. Zoezi la Wagombea na Kamati ya Uchaguzi kujulishwa uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF mnamo tarehe 20/11/2021. Wakati uchapishaji wa orodha ya mwisho ya wagombea na kutuma kwa wajumbe na kuhabarisha umma kwa ujumla 21/11/2021.

Wakili Benjamin alitangaza kuwa kuanzia 22-25 itakuwa ndiyo kipindi rasmi za wagombea waliofanikiwa kupita hatua zote kuanza kufanya kampeni na siku ya tarehe 27 ya mwezi Novemba, mwaka 2021 Uchaguzi Mkuu wa TPLB utafanyika rasmi Mkoani Kigoma.