Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Mechi Nne Zalindima Jumamosi na Jumapili Kwenye Viwanja Tofauti Tofauti

Ligi Kuu ya NBC imeendelea kutimua vumbi Jumamosi na Jumapili ambapo michezo kadhaa ya kuelekea kutamatisha ligi hiyo ilipigwa katika madimba tofautitofauti, huku baadhi ya timu zikiendeleza ubabe wakati nyingine zikizidi kuwa kwenye wakati mgumu kutokana na nafasi zilizopo na ugumu zinazokuta nao takribani katika kila mechi.

Mchezo wa kwanza ulipigwa Jumamosi ya tarehe 18 Juni, 2022 ulizikutanisha Geita Gold dhidi ya Biashara United mnamo majira ya 10:00 jioni ambapo timu ya Geita Gold ilifanikiwa kuibuka na alama 3 baada ya kuwaadhibu wapinzani wao kwa jumla ya mabao 2-0. Moja kati ya Magoli yaliyofungwa na timu hiyo lilifungwa na mshambuliaji wa Kitanzania George Mpole aliyefunga bao la kuongoza lililomfanya afikisha Magoli 16 sawa na mshambuliaji wa Young Africans Fiston Mayele aliyefanya hivyo kwenye mchezo uliopita; huku bao la pili likifungwa na Edmundi John.

Aidha, katika mchezo wa pili wa siku hiyo ya Jumamosi, Kagera Sugar aliwaalika Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Kaitaba; mechi hiyo ikipigwa majira ya saa 1:00 usiku ambapo timu hizo zilitoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1; bao la Dodoma jiji liwekwa kimiani na Waziri Junior (dkk 60) Kagera Sugar wakasawazisha kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mchezaji aitwae Abeid Athuman (dkk 83).

Katika hatua nyingine, siku ya Jumapili Juni 19, 2022 mchezo mwingine mkali ulipigwa kati ya Ruvu Shooting na Mbeya City; mchezo huo ulikuwa wa kufa na kupona kwani timu zote zilikuwa kama zimekamiana kufuatia umuhimu wa mchezo huo kwa kila timu. Hata hivyo, hali haikuwa nzuri kwa wenyeji Ruvu baada ya kuruhusu bao moja, lililofungwa na Baraka Mwalugunju kwenye kipindi cha mwisho; hata hivyo, kocha Charles Mkwasa bado anamatumaini ya kufanya vizuri katika michezo mingine.

Wakati hayo yakitokea huko kwa Ruvu, pale kwa Makapa Jijini Dar es Salaam, Simba waliendeleza ubabe wao kwa wakusanya kodi wa Kinondoni,(KMC) kwa kuwaadhibu jumla ya mabao3-1 na hivyo kufifisha matumani ya timu hiyo ya Halmashauri kumaliza wakiwa kwenye nafasi ya nne. Katika mchezo huo wa kiporo, KMC walikuwa moto zaidi kwenye dakika 45 za kwanza huku Simba wao wakirejea kwa kasi katika kipindi cha pili na kuwapelekea pumzi ya moto KMC ambapo wafanikiwa kurejesha bao walilokuwa wamefungwa na kuongeza mengine mawili yaliyopelekea mchezo huo kwisha 3-1.

Mabao ya Simba yalipachikwa na Kibu Dennis (dkk52), Pape Sakho (dkk 63) Henoc Inonga (dkk 66) huku bao la KMC likifungwa na Hassan Kabunda mnamo dakika ya 41 kipindi cha kwanza. Simba imefanikiwa kuifunga KMC mara mbili msimu huu ikifanya hivyo kwenye mzunguko wa kwanza katika mchezo ulipigwa kwenye dimba la Al Hassan Mwinyi Tabora, ilipoiadhibu timu hiyo jumla ya mabao manne (4).

Kufuatia matokeo ya michezo hiyo ya Jamamosi na Jumapili; Simba inasalia katika nafasi yake ya pili ikiwa na alama 57 baada ya kushuka dimbani mara 27, KMC wao wanabaki na alama zao 32 michezo 27; Mbeya City wanasogea hadi nafasi ya 7 wakiwa na alama 35 mechi 28; Geita Gold nao wanakwea mpaka nafasi ya 3 wakiwa na alama 42 baada ya kushuka uwanjani mara 28 pia wakati Ruvushooting wao wakiendelea kusalia kwenye nafasi yao ya 13 baada ya kukusanya alama 28 kwenye michezo 28.

Matokeo ya michezo hiyo ya siku za mwisho wa wiki yanaonesha jinsi ligi inavyoisha na ugumu wake kwani mpaka sasa bado mnyukano ni mkali kila timu ikihitaji alama tatu kwenye kila mchezo. Huku timu kongwe; Young Africans (Mabingwax28) na Simba (Mabingwa x22) ambazo zote zimeshuka dimbani mara 27, (alama 67) na nyingine (alama 57) nafasi zao zikiwa haziathiriwi na matokeo yeyote yale.

 

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.