Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Michezo 240 Kupigwa Ligi Kuu Msimu 2022/2023

Jumla ya michezo takribani 240 inatarajiwa kupigwa kwenye msimu ujao wa ligi kuu soka bara 22/23 ambapo jumla ya michezo 120 itapigwa nyumbani kwa kila timu huku mechi nyingine 120 zikipigwa ugenini.

Imetolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almasi Jumapili Kasongo Agosti 3, 2022 alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari za michezo kwenye mkutano uliofanyika Makao makuu ya TFF jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa kutakuwa na jumla ya mapumziko yasiyopungua 17 kwenye ratiba ya msimu mzima kulingana na baadhi ya matukio mengine yanayo weza kujitokeza wakati huo ikiwemo ratiba zinazo tolewa kwa mujibu wa kalenda ya FIFA na siku ya Augost 23,2022 ambapo ratiba itapisha wanafamilia wa soka kuungana na watanzania wengine kwenye zoezi zima la SENSA.

Aidha Almasi Kasongo aliongeza kuwa licha ya matukio hayo ratiba pia imeweza kuakisi kwenye baadhi ya mashindano mengine yakiwemo ya CHAN na AFCON ambapo wachezaji baadhi watakuwa na jukumu la kuungana na timu za Taifa, huku michuano mingine ikiwa ni ASCF na michuano ya Mapinduzi Cup ambapo pia timu nyingine za ligi kuu huwa zinashiriki kwenye michuano hiyo.

“Derby ya kwanza itapigwa kwenye mzunguko wa 8 ambapo itakuwa Oktoba 23, 2022 majira ya saa 11:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa” alisema Kasongo.

Hata hivyo alieleza pia ratiba za muda wa kuanza kwa mechi hizo ambapo kutakuwa na mechi zitakazo pigwa kuanzia majira ya saa 8:00 mchana mpaka saa 4:00 usiku kwa viwanja ambavyo vimefanyiwa maboresho yakiwemo ya kuwekwa taa.

Mechi 8 za awali mzunguko wa kwanza zitapigwa kuanzia Agosti 15, 2022 na kumalizika Agosti 17, 2022 ambapo mechi ya kwanza itawakutanisha Ihefu dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Highland Estate jijini Mbeya na mechi ya mwisho Azam wakikipiga dhidi ya Kagera Sugar majira ya saa 2:15 usiku kwenye uwanja wa Azam Complex.

Michezo itakayopigwa kwenye mzunguko wa 30 yote itapigwa Mei 27, 2023 ambapo Simba SC watamalizana na Coastal Union kwenye dimba la Benjamin Mkapa, huku Young Africans wenyewe wakifunga hesabu wakiwa ugenini dhidi ya wajela jela Tanzania Prisons majira ya saa 10:00 jioni.

 

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.