Timu Bora ni Golikipa; Mohammed Tajdin
Katibu wa Chama cha Makocha wa Mpira wa miguu Tanzania (TAFCA) Mohammed Tajdin amewataka wahitimu wa kozi ya ukocha wa magolikipa kwenda kuwapika magolikipa bora walio kwenye viwango vya kwenye ligi yetu inayozidi kukuwa na hata wengine kuweza kutumikia timu za Taifa.
Ameyasema hayo wakati wa kufunga kozi ya siku tano kwa makocha wa magoli kipa wa timu za Taifa, Ligi kuu ya NBC na Championship iliyoanza Agosti 05, 2022 Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF na kumalizika hii leo Agosti 09, 2022.
“Timu yoyote ili kuwa na rekodi nzuri inahitaji kuwa na goli kipa bora na mwenye uwezo, mpira wetu umekuwa sana huko nje ndio sababu TFF imekuwa ikijaribu kutilia mkazo kwenye kila eneo kwa nafasi yake ni wakati sasa nyinyi pamoja na sisi tuungane kutilia mkazo kwenye eneo hili la magolikipa.” Alisema Tajdin
Aliwapongeza wahitimu hao kwa kufahamu umuhimu wa fani hiyo huku akiwasisitiza kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliyojifunza na akitaka waamini vitu vidogo kwenye mpira ndio vinaweza kuuwa au kukuza mpira wetu, aliwashukuru pia wakufunzi wa kozi Haroon Amur Hamed akisaidiwa na Yusuf Abeid kwa kuacha majukumu mengine ili kushirikiana na TFF katika kulifanikisha hilo kwa lengo la kuweza kupiga hatua Zaidi kwenye mpira nchini kwetu.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wengine Kocha Josia Steven ameshukuru TFF kwa kuona umuhimu wa kuweza kuwaendeshea mafunzo ya aina hiyo kutokana na mahitaji kuwa mengi Zaidi huko nje kulinganisha na idadi ya makocha waliopo hapa nchini hasa wale wenye weledi na uhalali wa kufundisha timu.
Hata hivyo Josia ameomba utaratibu huo uwe ni endelevu kwa TFF kuzidi kuendesha mafunzo kwa makocha hao wazawa katika ngazi za juu Zaidi ili kuwaongezea wigo mpana wa kupata ajira kwenye timu zinazoshiriki ligi kuu ya NBC na hata kwenye timu za Taifa.
Washiriki 35 waliohitimu mafunzo hayo ni pamoja na; Soud Suleiman (Mtibwa Sugar),Adam Moshi (Dodoma jiji), Mansour Abdallah (African Sport), Eberhard Mhagama (Magnet Academy), Juma Kaseja (KMC FC), Steven Malashi (IST), Maimuna Mkane (Serengeti Girls), Fatuma Jawad (Serengeti Girls), Josia Steven (Timu ya Soka la Ufukweni), Issa Makumbo (Fountain Gate FC), Michael Mfaume (Fountain Gate Princess) na Ally Shomari (Big Stars).
Washiriki wengine ni; Kibwana Nyogoli (Allan Queens), Idd Mwinchum (Azam FC), Wilbert William (JKT TZ), Muharamy Sultan (Timu ya Taifa),Shaban Dihile (Green FC), Mussa Mbaya(Mbeya FC), Anna Joel(Simba Queens), Herry Boimanda(TZ Prisons), Emmanuel Kingu(KMC FC), SalimTupa(Coastal Union), Aswile Mwaikeno(Mbeya Kwanza), Patric Minangaya(Ihefu FC), Raphael Mpangala(African Sports), Emmanuel Mwansile(Polisi TZ), Bashiri Abdul(JMK Park), Mustapha Muembwa(Kilimani City), Abdul Ramadhani(Karume), Juma Mpongo, Mfaume Samata(Dodoma jiji), Mwanaharusi Abbas(Twalipo Academy), Abdulkarim Mtumwa(Twalipo Academy) na Aboaka Abdallah (Transit Camp).