Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Usanase Zawadi Apiga Hattrick

Mchezaji wa timu ya AS Kigali WFC ya nchini Rwanda inayoshiriki michuano ya Kufuzu Ligi ya Mabingwa wanawake ukanda wa CECAFA Usanase Zawadi (JZ 16) amepiga hattrick kwenye mchezo wao dhidi ya Warriors Queens FC ya visiwani Zanzibar.

Mchezo huo wa pili kundi A umepigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Agosti 18,2022 majira ya saa 1:00 usiku na kumalizika kwa timu ya AS Kigali WFC kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 yote yakifungwa na mchezaji Usanase Zawadi.

Usanase anafikisha jumla ya mabao 5 kwenye michuano hiyo sawa na mchezaji Madina Awol Busser (JZ 09) anaye chezea kikosi cha timu ya Commercial Bank FC, kinara wa mabao kwenye michuano hiyo mpaka sasa ni Loza Abera Geinore nahodha wa kikosi cha CBE akifikisha jumla ya mabao 8.

Hata hivyo kwa upande wa timu ya Warriors Queens FC licha ya kukubali kichapo hicho dhidi ya AS Kigali WFC imeonekana kuimarika zaidi na kuwa bora kulinganisha na mchezo wao wa awali waliopoteza dhidi ya CBE FC ya Ethiopia kwa magoli 9-0.

Mlinda mlango wa timu ya Warrios Queens FC Tausi Swalehe Abdallah ambaye pia aliwahi kuidakia timu ya Taifa ya wanawake Tanzania alionekana kuwa bora zaidi akiokoa michomo mingi iliyojaribu kufika kwenye lango lake na kuinusuru timu yake kufungwa magoli mengi.

Kundi A litakamilisha hesabu zake kwenye hatua ya makundi jumapili Agosti 21, 2022 timu ya Warriors Queens itakapo shuka dimbani kujiuliza dhidi ya FOFILA PF ya nchini Burundi ikiwa timu zote hizo zimepoteza kwenye mechi zao za awali.

Mchezo mwingine wa kundi A utawakutanisha kinara wa kundi Commercial Bank FC dhidi ya AS Kigali WFC wote wakiwa na alama sawa isipokuwa idadi ya magoli timu ya CBE wenyewe wakiongoza kwa magoli 14, tofauti ya magoli 9 na AS Kigali WFC wenye jumla ya magoli 5 wakishikilia nafasi ya pili kundi A.

 

 

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.