Shime: Tunakwenda kutetea ubingwa wetu
Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ Bakari Shime amesema kikosi chake kipo tayari kutetea ubingwa wa michuano ya wanawake ukanda wa Afrika Kusini ( Hollywood bets Cosafa women’s championship) inayoendelea kutimua vumbi katika mji wa Port Elizabeth, Afrika Kusini.Kocha huyo ameyasema hayo leo Agosti 01,2022 kuelekea katika mchezo wa kwanza Kwa ‘Twiga Stars’ utakaowakutanisha na timu ya taifa ya Comoro siku ya Ijumaa Septemba 02,2022 majira ya saa 6:00 mchana katika uwanja wa Madibaz.”Hii ni mara ya kwanza Kwa Tanzania kuingia katika michuano hii akiwa bingwa mtetezi tofauti na miaka ya nyuma hivyo ninafahamu kwamba michuano itakuwa migumu kwakuwa timu zote ni nzurii na zina wachezaji wenye viwango Bora. Jambo la muhimu kwetu ni kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri na kurudisha Kombe nyumbani”. Alisema kocha Shime.Kocha aliongeza kuwa , Mbali na kutetea ubingwa huo, michuano ya Cosafa itawapa uzoefu na watajifunza mengi kutoka Kwa timu za ukanda wa cosafa ambazo zimepiga hatua akitolea mfano timu ya Afrika kusini pamoja na Zambia ambazo zote zimefuzu kushiriki Kombe la dunia mwakani. Ninashukuru uongozi wa Cosafa Kwa kuendele kutupa mualiko ikiwa ni mara ya nne mfululizo na mara zote Tanzania imekuwa ikifanya vyema, niwaombe watanzania na wapenzi wa soka kuendela kuiombea timu ya Twiga Stars. Michuano ya Cosafa imeendelea tena Leo Kwa michezo miwili ya kundi B kupingwa ukiwakutanisha timu ya Lesotho dhidi ya Eswatini na Lesotho kuibuka na ushindi wa Goli 3-0 wakati Zambia nae akipata ushindi wa Goli 2-0 mbele ya Namibia. Timu mwenyeji Afrika Kusini akianza vyema katika mchezo wa ufunguzi baada ya kumchakaza Angola Goli 2-0.