Kocha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” Honour Janza ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoingia kambini kwa michezo miwili ya Kirafiki kwenye Kalenda ya FIFA dhidi ya Libya.

Kikosi kitaingia kambini Jumamosi Septemba 17, 2022 jijini Dar es salaam.

Wachezaji 23 waliotajwa kuunda kikosi hicho ni Aishi Manula na Beno Kakolanya (Simba), Kibwana Shomari (Young Africans), Saidi Kipao , Datius Peter na David Luhende (Kagera Sugar); Abdulmalick Adam (Namungo FC), Abdi Banda (Chippa United, Afrika Kusini), Carlos Protas (Tusker FC-Kenya), Oscar Masai (Geita Gold), Dickson Job (Young Africans) na Abdallah Mfuko kutoka Kagera Sugar.

Wengine ni Himid Mao Mkami (Ghazl ElMahalla-Misri), Sospeter Bajana (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Feisal Salum (Young Africans), David Uromi (Moroka Swallows- Afrika Kusini) Mohammed Issa Banka (Namungo FC), Mbwana Samatta-Genk-Ubelgiji), Simon Msuva (Al-Qadsiah FC- Saudi Arabia), Ibrahim Joshua (Tusker fc-Kenya), Said Khamis (Hatta Club- UAE) na Habib Kiyombo (Simba SC).

Timu inatarajia kuondoka Jumanne Septemba 20, 2022.