Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Singida Big Stars Yagoma Kuachia Alama 3 kwa Simba

Timu ya Singida Big Stars (SBS) ilishuka kumenyana na miamba wa soka nchini Simba Sport Club ya Dar es Salaam kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Liti uliopo mjini Singida ambapo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1.

Mmchezo huo uliopigwa Novemba 09, 2022 majira ya saa 10:00 jioni wenyeji Singida BS ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa kiungo mshambuliaji wao Deusi David Kaseke (27) mnamo dakika ya 10 kipindi cha kwanza huku Simba wao wakisawazisha bao hilo kunako dakika ya 59 ya mchezo, kupitia kwa Peter Banda (11) aliyetoka katika benchi baada ya Jonas Mkude kwenda nje.

Akitoa tathimini ya mchezo huo Kaimu kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda alikiri kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu na kwamba kikosi chake kimecheza vizuri licha ya kutanguliwa kufungwa walikwenda kwenye mapumziko na kuelekezana nini cha kufanya katika kipindi cha pili jambo amablo anashukuru kuwa wachezaji wake walilifanya kwa umakini mkubwa hatimaye kusawazisha bao hilo.

Mgunda alieleza zaidi kuwa ligi ni ngumu na kwamba kila mchezo unastaili yake ya namna ya kuucheza lakini kuna mambo mazuri yaliyoonekana kwenye mchezo huo ambayo ameahidi kutaendeleza zaidi huku akidai kwenda kuyafanyia kazi makosa yote kwa kurekebisha ili kwenye michezo mingine timu iweze kupata matokeo mazuri zaidi.

Naye kocha msaidizi wa Singida Big Stars, Martin Lule alieleza kuwa kikosi chao kimefanya vyema kwenye mchezo huo japokuwa matokeo hayo yalikuwa ni nje na malengo yao. Kuhusu suala la ubora wa timu aliyokutana nayo, Lule alisema kuwa yeye anachojua kila timu inayoshiriki ligi kuu Bara ni bora, hivyo walifahamu uwezo wa Simba na kuichukulia kawaida kama wanavyokuwa kwenye michezo mingine yote ya ligi.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Singida Big Stars kukutana na Simba kwenye mchezo wa ligi kuu baada ya kuwa imepanda daraja msimu huu wa 2022/2023. Kwa matokeo ya mcheozo huo uliopigwa katika uwanja wa Liti Singida, Simba inafikisha michezo 9 ikikusanya alama 18; alama mbili nyuma ya vinara Young Africans, wakati Singida Big Stars nao wanafikisha alama 18 pia, baada ya kushuka dimbani mara 10.

Katika mchezo mwingine Azam FC iliwakaribisha Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, mchezo uliopigwa majira ya saa 1:00 usiku. Katika Matokeo ya mchezo huo timu ya Azam FC iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kuifanya Azam kupanda hadi kwenye nafasi ya pili baada ya kushuka dimbani mara 10, na kukusanya jumla alama 20 sawa na vinara Young Africans, wakitofautina kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.

 

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.