Simba Yatinga Robo Kibabe, Young Africans Nayo Yaifuata
Timu za Simba na Young Africans zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya timu hizo kupata ushindi kwa katika michezo tofauti iliyopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Machi 18 na 19, 2023.
Simba ilitangulia kutinga robo fainali Klabu Bingwa Afrika baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi Horoya AC katika mchezo uliopigwa siku ya Jumamosi ya Machi 18, 2023 huku Young Africans nao wakifanya hivyo kwa kulipa kisasi cha bao 2-0 dhidi ya US Monastir ya Tunisia na kufanikiwa kuongoza kundi D, wakisubiri mchezo mmoja wa mwisho utakao wakutanisha TP Mazembe ya Kongo.
Magoli ya Simba yalipachikwa wavuni na Clatous Chota Chama matatu (3), Jean Baleke (2), Sadio Kanoute (2); magoli hayo yalifungwa mnamo dakika ya 10, 32, 36, 55, 65, 70 na dakika ya 87 huku Young Africans wao wakifunga mabao yao dakika ya 32 Kennedy Msonda na Fistone Mayele aliyepachika bao lake mnamo dakika ya 59 ya mchezo.
Baada ya mchezo hiyo, timu zote zinafanikiwa kukata tiketi ya kutinga robo fainali, ambapo Simba imefikisha alama 9 na kushika nafasi ya pili wakati Young Africans wao wakiwa na alama 10 wakiongoza kundi lao. Hata hivyo, timu ya Young Africans inaweza kumaliza hatua ya makundi ikiwa katika nafasi ya kwanza endapo itafanikiwa kushinda Kwa mabao Mengi kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya TP Mazembe na kama US Monastir watapoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Real Bamako.
Wakati Young Africans wakiendelea kuomba Dua jema kwao huku wakiomba Dua mbaya kwa Monastir dhidi ya Bamako wakati watani wao Simba wao wakiwa kwenye nafasi ya pili ambayo ikipata ushindi dhidi ya Raja C, bado haiwezi kuzipita alama za wababe hao kutoka Morocco kwani tayari timu hiyo ina alama13 ikifuatiwa na Simba yenye alama 9 za CAF.
Ushindi wa watani wa jadi umechegizwa na motisha kutoka kwa Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeahidi kununua kila goli kwa TSh. 5,000,000 Milioni Tano hali iliyopelekea watani hao kushinda a kuzivuna pesa za MAMA.