JKT Queens Kileleni Raundi ya Tatu TWPL

Mechi za raundi ya tatu Ligi kuu ya Wanawake zimemalizika Januari 3, 2024 kwa kupigwa mechi tano zote huku JKT Queens ikiwa ndio timu iliyomaliza raundi hiyo kileleni baada ya ushindi wa magoli meng zaidi.

JKT Queens ilipata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Amani Queens ambao ulimalizika kwa mwenyeji Amani Queens kupoteza kwa 0-10, matokeo yaliyo iweka JKT Queens kileleni kwa jumla ya alama 9 na jumla ya magoli 15 wakiwa hawajaruhusu bao lolote.

Mbali na JKT Queens kuongoza ligi wanafuatiwa na Simba Queens ambayo pia imepata ushindi kwenye mchezo wake dhidi ya Yanga Princess uliomalizika kwa matokeo ya 3-0 Januari 3, 2024. Simba Queens imelingana alama na JKT Queens tofauti ikiwa magoli, Simba imefunga magoli 11 na kuruhusu magoli 3.

Matokeo mengine Alliance Girls 0-1 Fountain Gate Princess, Ceasiaa Queens 2-1 Geita Gold Queens, Baobab Queens 0-1 Bunda Queens.

Michezo mingine ya raundi ya nne ligi kuu ya wanawake inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi Januari 9 na 10, 2024.