Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Afanya Ziara TFF Kigamboni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Suleiman Serera amefanya Ziara ya kitembelea kituo cha ufundi cha TFF, kilichopo Kigamboni Dar es salaam Julai 25, 2024 ambapo Ziara hiyo yote ikiongozwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu TFF Kidao Wilfred.
Kwenye Ziara hiyo iliyoambatana na kikao na majadiliano marefu kati ya wawili hao, pia waliweza kuzungukia maeneo mbalimbali ya majengo yaliyoko kwenye kituo hiko sambamba na viwanja vyote viwili vya mpira wa miguu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Suleiman Serera aliipongez TFF Kwa juhudi inazoweka kwenye usimamiaji na uendeshaji wa masuala mbalimbali wanayojihusisha nayo.
Serera alisema chochote kinachofanywa na TFF katika kuleta maendeleo ya mpira wa miguu serikali itaendelea kuunga mkono kwani matunda mazuri yatakayo patikana ni Neema ya Taifa la Tanzania Kwa ujumla.
“Tumeona utofauti wa TFF na Mashirikisho mengine katika usimamizi na uendeshaji wa taratibu mbalimbali, hivyo nitoe rai Kwa hayo mashirikisho kuja kuchukua ujuzi na maarifa ya namba nzuri ya usimamizi ili sote tuweze kisonga mbele” alisema Serera.
Kwa upande wa mwenyeji wa ziara hiyo Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono masuala mbalimbali yanayofanywa na TFF, aidha alisema ugeni huo ni faraja Kwa TFF kwani ni jambo kubwa kuweza kupata muda wa kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ndani ya TFF na mpira wa miguu Kwa ujumla.
“Kwangu Mimi kikao hiki ni miongoni mwa vikao muhimu, na chenye thamani kubwa ambapo nategemea kupitia kikao hiki tutakwenda kuongeza chachu kwenye maeneo mbalimbali ya kushughulikia ndani ya Taasisi” alisema Katibu Mkuu TFF.
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Suleiman Serera alisema mbali na kutembelea kituo hiko pia anampango wa kuweza kufika kutembelea pia kituo kingine cha ufundi cha TFF kilichopo Mnyanjani Tanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Afanya Ziara TFF Kigamboni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Suleiman Serera amefanya Ziara ya kitembelea kituo cha ufundi cha TFF, kilichopo Kigamboni Dar es salaam Julai 25, 2024 ambapo Ziara hiyo yote ikiongozwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu TFF Kidao Wilfred.
Kwenye Ziara hiyo iliyoambatana na kikao na majadiliano marefu kati ya wawili hao, pia waliweza kuzungukia maeneo mbalimbali ya majengo yaliyoko kwenye kituo hiko sambamba na viwanja vyote viwili vya mpira wa miguu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Suleiman Serera aliipongez TFF Kwa juhudi inazoweka kwenye usimamiaji na uendeshaji wa masuala mbalimbali wanayojihusisha nayo.
Dkt.Serera alisema chochote kinachofanywa na TFF katika kuleta maendeleo ya mpira wa miguu serikali itaendelea kuunga mkono kwani matunda mazuri yatakayo patikana ni Neema ya Taifa la Tanzania Kwa ujumla.
“Tumeona utofauti wa TFF na Mashirikisho mengine katika usimamizi na uendeshaji wa taratibu mbalimbali, hivyo nitoe rai Kwa hayo mashirikisho kuja kuchukua ujuzi na maarifa ya namba nzuri ya usimamizi ili sote tuweze kisonga mbele” alisema.
Kwa upande wa mwenyeji wa ziara hiyo Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono masuala mbalimbali yanayofanywa na TFF, aidha alisema ugeni huo ni faraja Kwa TFF kwani ni jambo kubwa kuweza kupata muda wa kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ndani ya TFF na mpira wa miguu Kwa ujumla.
“Kwangu Mimi kikao hiki ni miongoni mwa vikao muhimu, na chenye thamani kubwa ambapo nategemea kupitia kikao hiki tutakwenda kuongeza chachu kwenye maeneo mbalimbali ya kushughulikia ndani ya Taasisi” alisema Katibu Mkuu TFF.
Hata hivyo Dkt.Suleiman Serera alisema mbali na kutembelea kituo hiko pia anampango wa kuweza kufika kutembelea pia kituo kingine cha ufundi cha TFF kilichopo Mnyanjani Tanga.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.