Timu ya Soka la ufukweni yashiriki mashindano ya Casablanca Cup, Morocco
Timu ya Taifa ya Soka la ufukweni imeshiriki mashindano ya Casablanca Cup yaliyofanyika nchini Morocco katika mji wa Casablanca.
Timu hiyo ilipata nafasi ya kucheza michezo mitatu ya kimataifa ambapo ilikutana na timu ya Ufaransa katika mchezo wake wa Kwanza uliochezwa Agosti 16, 2024 na kupoteza mchezo huo kwa goli 2-3. Mchezo wa pili walicheza na timu mwenyeji Morocco ambapo pia walipoteza katika mchezo huo.
Mchezo wa mwisho ulichezwa Agosti 18, 2024 Tanzania dhidi ya Belgium na mchezo ulimalizika Kwa sare ya goli 6-6.
Ushiriki wa Tanzania katika mashindano ya Casablanca Cup ni sehemu ya maandalizi ya timu ya Taifa ya Soka la ufukweni kuelekea katika mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa upande wa soka la ufukweni (BAFCON) , 2024 yatakayofanyika nchini Misri yakijumuisha nchi nane za ukanda wa Afrika zilizofuzu katika mashindano hayo mwaka huu.
Mashindano ya Cassablanca Cup yamejumuisha timu nne kutoka Morocco, Belgium, Ufaransa na Tanzania ambayo yalianza Agosti 16 na kumalizika Agosti 18, 2024.