Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Etienne Ndayiragije amefanya mabadiliko madogo katika kikosi kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi.
Wachezaji walioondolewa katika kikosi kwasababu ya kuwa majeruhi ni David Mwantika,Aishi Manula na Ibrahim Ajibu ambao nafasi zao zinazibwa na Mohamed Ally Yusuf(Lipuli),Oscar Godfrey Masai(Azam FC) na Haruna Shamte(Lipuli)
Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inatarajia kushuka dimbani Jumapili dhidi ya Kenya katika Uwanja wa Kasarani,Kenya kusaka nafasi ya kufuzu hatua inayofuata ya michuano ya CHAN.
Mchezo wa Kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa ulimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0-0