Azam Yakwea Kileleni, Dodoma Jiji Yavuna Ushindi Mbele ya KMC

Ligi Kuu Bara iliendelea Novemba 15, 2022 kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja viwili tofauti ambapo mchezo wa saa 10:00 jioni uliwakutanisha KMC dhidi ya Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Uhuru uliopo Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza mwenyeji KMC alikubali kichapo cha bao 2-1 kilichowashangaza wao wenyewe lakini pia baadhibya wadau wa soka ambao waliamini kuwa kutokana na KMC kuonesha kiwango bora kwenye mechi za hivi karibuni huenda a dereva kupata matokeo katika mchezo huo jambo ambalo halikutokea.

Magoli yote ya Dodoma Jiji yalifungwa katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Seif Rashid huku  KMC wao wakifanikiwa kuandika bao  katika  kipindi cha pili kupitia kwa Solomon Anderson.

Makocha waote walizungumzia mchezo huo Kassim Lyogope wa Dodoma Jiji aliwapongeza wachezaji wake na kusema wamecheza kwa kujituma na umakini mkubwa huku akionesha kuridhishwa na kiwango kilichooneshwa na timu yake. Alisema sasa mbinu zake zinaanza kueleweka kwa wachezaji hao na kwamba anaaminibkuwa kadri siku zinavyokwenda ndivyo mashabiki wa timu hiyo watarajie makubwa na mazuri zaidi.

Kwa upande wake Ahmad Ally kocha msaidizi wa KMC alisema kikosi chao kilikuwa na uchovu ndiyo sababu kubwa iliyopelekea wao wasicheze vizuri hasa katika kipindi cha kwanza. Kocha huyo aliongeza kuwa pamoja na kutocheza vizuri bado kiliweza kutengeneza nafasi za magoli japokuwa hazikuzaa matunda huku akibainisha kwamba kilichotokea ni hali ya kawaida katika mchezo wa mpira wa muguu.

Ally Alieleza kuwa makosa machache waliyoyafanya wachezaji wake ndiyo yaliyoigharimu timu kupoteza mchezo huo, na hivyo kuahidi kuyafanyia kazi makosa hayo ili kuweza kupata matokeo mazuri kwenye michezo mingine inayofuata.

Katika mchezo mwingine uliopigwa majira 01:00 usiku kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi ; Azam FC waliwakaribisha Ruvushooting ” Barcelona ya Bongo” ambapo timu ya Azam iliweza kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 . Bao la Azam FC lilipatikana katika kipindi cha pili (dakika ya 74 ) kwa mkwaju wa penati iliyoenda kupigwa na Idris Mbombo kuwafanya Azam kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi.

Kwa matokeo hayo Azam anafikisha alama 26 akishikilia nafasi ya kwanza kwenye ligi baada ya kucheza michezo 12 akiwaacha Simba na Young Africans ambao wanaviporo vya michezo ya Ligi Kuu Bara; Simba anamichezo miwili 2 mkononi wakati  Young  Africans wao wakiwa na michezo 3 mkononi.