Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura amefafanua kuhusu timu zilizoshuka Daraja baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Wambura amesema timu ya African Lyon na Stand United zimeshuka Daraja kwenda Daraja la Kwanza wakati Kagera Sugar na Mwadui zitacheza Mtoano na timu za Daraja la Kwanza kupata timu mbili zitakazocheza Ligi Kuu na mbili zitakazocheza Ligi Daraja la Kwanza.

Akizungumzia tukuo la kukosewa kwa takwimu kwenye msimamo wa mwisho wa Ligi Kuu,Wambura ameomba radhi na kusema Bodi ya Ligi itachukua hatua kwa Mtunza Kumbukumbu.

Kwa ufafanuzi huo sasa Pamba watacheza na Kagera Sugar Uwanja wa Nyamagana wakati Geita Gold FC watakua nyumbani Nyankumbu kuwakaribisha Mwadui katika mechi zitakazochezwa Juni 2,2019 na maridiano kuchezwa Juni 8,2019 kwenye Viwanja vya Mwadui Complex na Kaitaba.