Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

CAF C Diploma Imefunguliwa Makao Makuu TFF

Kozi ya walimu wa mpira wa miguu ngazi ya CAF C Diploma inayojumuisha washiriki 45 imefunguliwa na Makamu wa kwanza wa Rais TFF Athumani Nyamlani Julai 29, 2022 makao makuu ya Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo Nyamlani amewatakia kila lakheri washiriki hao kwenye kipindi chote cha mafunzo yao, pamoja na wakati ambao watakwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo kwenye sehemu zao za kazi.

Alisema kuwa moja ya lengo kubwa la TFF ni kuendeleza mpira wa miguu nchini, hivyo kwenye kufikia maendeleo hayo makocha wanapaswa kujitoa kwenye kuandaa vipaji vya wachezaji wapya kuanzia umri mdogo Zaidi (Youth Football Development).

Aidha amewataka washiriki hao wakawe ni mfano bora kwa makocha wengine huko nje kwa kuepuka kwenda kinyume na kanuni na sheria za mpira wa miguu zinavyowataka hususani kuepuka kuwa na upendeleo kwa baadhi ya wachezaji kutokana na majina wa watu Fulani.

Makamu huyo wa Rais TFF alisema kufanya hivyo kwa baadhi ya makocha kunatafsiriwa kuwa ni kitendo cha rushwa kwani inaaminiwa upendeleo wa aina yoyote kwenye mpira ni rushwa, hivyo hata kumpatia nafasi kubwa mchezaji mmoja kwenye kila mechi hata kama kazidiwa kiwango na wachezaji wengine ambao hawapatiwi nafasi pia ni upendeleo.

Kozi hiyo ya miezi mitatu imeanza Julai 25, 2022 na inatarajiwa kuwa na moduli 3 kwenye muda wote huo ambapo moduli ya kwanza iatakuwa na jumla ya siku 10 na baada ya hapo washiriki hao watakwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo kwa vitendo kwenye vituo vyao vya kazi.

Washiriki 45 wanaoshiriki mafunzo hayo ni; Aloyce Mathew, Mohammedi Abdallah, Isaya Mganda, Abdallah Mbonde, Frank Faraja,Joshua Charles, Armstrong Clement, Joseph Christian, Monja Liseki, Kisa .L. Peter, Mussa Namkoveka, Hilali Uwesu, Shabani Bakari,Ali Khamis, Maimuna Hamu, Adelard Mishinga, Khalifa Omary,Ramadhani Juma, Yahya Salum na Omari Matwiko.

Wengine; Henry Hezron, Juma Mohammed, Sylvester Aldor, Haji Ali, Matoka Ahmad, Kulinganila Kulinganula, Newland Kisyeri, Athumani Athumani, Sitta Shija, Katungunya Katungunya, Dickens Edgar, Said Abdallah, Titho Kithojo, Rich Oscar, Hassan Juma, Joseda Patrick, Henry Shindika, Amri Kiemba, Victor Hussein, James Haule, Athuman Idd, Yusuph Mohamed na James Mhagama.

 

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.