CECAFA 2022 Kuzinduliwa Rasmi Benjamin Mkapa
Michuano ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake kanda ya CECAFA (CAF Women’s CL Qualifiers CECAFA Zone) imeanza kutimua vumbi rasmi Agosti 14, 2022 kwa kupigwa mechi mbili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mechi ya awali kati ya SHE Corporates ya nchini Uganda na timu ya YEI Joints Stars majira ya saa 10:00 jioni ilimalizika kwa timu mwenyeji kupata ushindi wa magoli 6-0, huku Simba Queens wenyewe wakianza vizuri kwa kumchapa magoli 6-0 timu ya Grade Republicaine.
Miongoni mwa viongozi waliohudhulia kwenye ufunguzi huo ni pamoja na Rais wa CECAFA ambaye pia ni rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania Wallace Karia, huku akiambatana na makamu wa pili wa rais Steven Mnguto na viongozi wengine.
Michezo inayofuata itapigwa Agosti 15, 2022 kwenye uwanja wa Azam Complex, wakishuka dimbani Commercial Bank FC dhidi ya Warriors Queens majira ya saa 10:00 jioni, huku timu ya Fofila PF wakikipiga dhidi ya AS Kigali WFC majira ya saa 1:00 usiku.
Michuano ya SECAFA inahusisha timu 8 kutoka mataifa tofauti za ukanda huo, huku Tanzania ikiwakilishwa na Simba Queens na Warriors Queens kutoka visiwani Zanzibar. Timu nyingine ni SHE CORP, Y.J.STARS, GRFC, Commercial Bank FC, Fofila PF na AS Kigali.