Dirisha Dogo la Usajili kwa Klabu za Ligi Kuu,Daraja la Kwanza na Daraja la Pili linafungwa Disemba 15, 2018 saa 5:59 usiku

Klabu zinakumbushwa kutuma orodha ya wachezaji waliowaongeza katika dirisha dogo.

Wakati wa dirisha dogo klabu inaruhusiwa kuongeza idadi ya wachezaji kama haikusajili wachezaji 30 wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha kubwa.

Klabu ikimtoa mchezaji kwa mkopo haitoi nafasi ya kusajili mchezaji mwingine,mchezaji aliyetolewa kwa mkopo bado ni mchezaji wa klabu husika.

Dirisha dogo linatumika kujaza nafasi za wachezaji kama hawakutimia 30 wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha kubwa na kwa wale waliomaliza mkataba na klabu.