Timu ya Taifa ya wanawake ya Djibouti imekubali kipigo cha bao 12 mbele ya Timu ya Kenya katika michuano ya CECAFA ya wanawake inayoendelea Uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo Kenya wamepata Hat trick tatu kutoka kwa Mercy Airo ambaye alitokea benchi akifunga dakika ya 53, 61 na 65 huku Jentrix Shikangwa ambaye amefunga goli nne dakika ya 14, 16, 56 na 85 huku Mwanalima Jereco magoli dakika ya 34, 86 na 90 na magoli mengine yakiwekwa nyavuni na Vivian Makokha dakika ya 3 na Jamet Bundi dakika ya 45.

Kwa matokeo hayo yameshaashiria wazi kuwa Djbouti ameshatupwa nje ya michuano hiyo kwa jumla ya bao 26.