Dodoma Jiji Yazinduka na Kuichapa Coastal Union Mkwakwani Tanga

Timu ya Dodoma Jiji ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa Novemba 30, 2022 majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Mkwakwani Tanga na kuicha Coastal Union katika tafakuri ya kilichotokea uwanjani hapo.

Coastal Union licha ya kuonesha kiwango bora uwanjani bado haikuweza kupata ushindi mbele ya walima Zabibu kutoka Dodoma. Pamoja na Coastal Union kuwa moto zaidi katika mchezo huo, haikuwa kikwazo kwa Dodoma Jiji kuibuka kidedea.

Bao la Dodoma Jiji lilipatikana mwishoni mwa mchezo, mnamo dakika ya 89 bao hilo likifungwa na Rashid Chambo, mchezaji wa zamani wa Coastal Union aliyetimkia Dodoma Jiji.

Coastal Union italazimika kutafuta matokeo chanya kwenye michezo yake miwili iliyosalia kwenye duru ya kwanza kuanzia mechi moja ikiwa ya Jumosi Disemba 3, 2022 dhidi ya Simba, timu ambao kwa sasa inashauku ya kupata matokeo mazuri ili kuweza kumaliza wakiwa kileleni mwa ligi Kuu ya NBC. Hivyo Wagosi wa Kaya watakuwa na kibarua kigumu cha kwenda kuwazuia Wanamsimbazi hao kupata alama 3.

Kufuatiaa matokeo hayo yq mchezo uliopita kati Coastal Union na Dodoma Jiji; Dodoma inasogea hadi nafasi ya 13 ikiishusha Ihefu kwenye nafasi hiyo na kuipeleka kwenye nafasi ya 14 ikiwa na alama 12 baada ya kushuka dimbani mara 14.