Fainali za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa RCL zinataraji kupigwa Kesho kwenye Uwanja wa Halmashauri Bariadi.

Mchezo huo wa Fainali utazikutanisha timu za DTB FC na Pan Africans zote za Dar es Salaam.

Pan Africans wameingia hatua hiyo ya Fainali baada ya kuishinda Isanga Rangers FC ya Mbeya kwenye mchezo wa nusu fainali kwa mabao 2-0 wakari DTB FC yenyewe ikipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbuni FC ya Arusha.

Mchezo wa mshindi wa tatu utazikutanisha timu za Isanga Rangers FC na Mbuni FC.

Mechi zote zitachezwa Uwanja wa Halmashauri Bariadi ambapo ule wa mshindi wa tatu ukianza saa 7 mchana ukifuatiwa na Fainali saa 9 mchana.

Mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu watapanda Ligi Daraja la Pili 2019/2020.