Fainali za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoendela mkoani Simiyu,katika uwanja wa Halmashauri Bariadi imeshuhudia DTB FC ya Dar es Salaam ikipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Top Boys FC ya Ruvuma.

Gabriel Ndimbo alianza kuiandikia bao la kuongoza Top Boys katika dakika ya 10 kabla ya DTB hawajasawazisha katika dakika ya 14 kupitia kwa Haddo Akida aliyepokea pasi kutoka kwa Jumaa Jumaa, na katika dakika ya 23 Omary Mkwawa akaipatia DTB bao la ushindi kwa 23 mkwaju wa penati baada ya Dickson Samson kuangushwa eneo la hatari.

Mchezo huo Kamishna alikua Judith Gamba kutoka Dodoma, Muamuzi wa katikati Tatu Malogo kutoka Tanga, Muamuzi msaidizi namba moja Felix Sosthenes kutoka Mbeya, Muamuzi msaidizi namba mbili Mohammed Msengi kutoka Pwani na Muamuzi wa akiba Ahmed Aragija wa Manyara.

Katika mchezo wa pili Isanga Rangers FC ya Mbeya ilifanikiwa kumchapa mwenywji Bariadi United FC kwa mabao 2-0.

Mabao ya Isanga yalifungwa na Aplay Kongoa dakika ya 72 na Devis Kakuyu katika dakika ya 80 wakati lile la kufutia machozi la Bariadi likifungwa na Mwakibose Gwakisa katika dakika ya 21.

Kamishna wa mchezo alikua Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga, Muamuzi wa katikati Amina Kyando wa Morogoro, Muamuzi msaidizi namba moja Gidion Nyansio kutoka Katavi, Mwamuzi msaidizi namba mbili Rajabu Ally wa Morogoro na Muamuzi wa akiba Abel William wa Arusha.

Kesho fainali hizo zinaendelea kwa michezo miwili itakayochezwa Uwanja wa Halmashauri, kuanzia saa 8 mchana.