Fainali za Vijana wa U20 Zaendelea Kutimua Vumbi

Fainali za Ligi Kuu ya vijana wa U20 kwa msimu 2020/2021 zimendelea June 11 , 2021 ambapo michezo miwili ilichezwa kwenye uwanja wa Azam Complex , Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza uliwakutanisha vijana wa Tanzania Prisons dhidi ya timu ya vijana ya Kagera Sugar; mchezo ambao ulimalizika kwa timu ya Tanzania Prisons kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mabao hayo ya Tanzania Prisons yalipachikwa kimyani na Kelvin Abesalon dakika ya 36 na badaye, mnamo dakika za mwisho za mchezo kuongeza la pili.

Mchezo wa pili uliokuwa ukisubiriwa na watu wengi, uliwakutanisha timu ya Azam FC ya vijana wa U20 dhidi ya timu ya vijana ya Mtibwa FC, mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu tasa licha ya timu ya vijana ya Azam FC kuwa na umiliki mkubwa lakini vijana wa Mtibwa walihakikisha wanajilinda vya kutosha.

June 12, 2021 ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili ambapo mchezo wa kwanza utawakutanisha Yanga Africans dhidi ya JKT Tanzania majira ya saa 1 usiku huku mchezo wa pili ukiwakutanisha timu ya vijana ya Simba SC dhidi ya vijana wa Mwadui FC.