Fountain Gate Academy Yaanza Vyema Mashindano ya Shule Afrika

Timu ya Fountain Gate Dodoma imeanza vyema mashindano ya African Schools Championship huko Durban nchini Afrika Kusini baada ya kupata ushindi mbele ya wenyeji wa mashindano hayo Adendale Technical.

Fountain Gate Academy imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Adendale Technical kwenye mchezo wao wa awali kundi A uliopigwa kwenye uwanja wa King Zwelithini Aprili 5, 2023; magoli 5 yakifungwa na Winfrida Hubert na mengine mawili yakifungwa na Mary Siyane.

Ikumbukwe Fountain Gate Academy ilifanikiwa kutinga fainali hizo baada ya kubeba ubingwa kwenye hatua za awali zilizohusisha timu za ukanda wa CECAFA zilizofanyika hapa nchini mwezi Agosti mwaka jana.

Fountain Gate Academy ipo kwenye kundi ‘A’ ambalo wamepangwa na wenyeji wa fainali hizo Adendale Technical na Scan AID

Miongoni mwa viongozi walioambatana na Fountain Gate kwa lengo la sapoti na kushuhudia fainali hizo ni pamoja na Rais wa CECAFA ambaye pia ni rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania Wallace Karia, sambamba na Naibu Waziri Sanaa Utamaduni na Michezo Hamisi Mwinjuma pamoja viongozi wengine.