GIFT Yapangwa Kwenye Makundi Mawili
Mashindano mapya ya CAF ya wasichana U17 ya Integrated Football Tournament (GIFT) yaliyotambulishwa hivi karibuni Afrika, yanayotarajia kuanza kutimua vumbi kwa mara ya kwanza mwenyeji akiwa Tanzani kuanzia Januari 7-18 kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es salaam.
Ni baada ya droo iliyochezeshwa Januari 4, 2025 kuweka bayana makundi Mawili yatakayo tumika kwenye ratiba ya mashindano hayo, huku timu mbili kutoka Tanzania (TDS na JKT Queens zikiwq kwenye makundi tofauti.
Wakati TDS ikijipanga kuwakabili kundi B. Concili Girls (Uganda), Aigle Noir FC (Burundi) na Hilaad FC ya (Somalia), timu ya JKT Queens yenyewe inakibarua cha kundi A ambapo itacheza na City Light FA (Sudani Kusini),B.D Kenema FC (Ethiopia) na K.A.S FC (Kenya).
Akizungumzia Makundi hayo kocha Mkuu timu ya kuendeleza vipaji TDS Wasichana U17 Bakari Shime alisema ni mapema kutoa tathmini ya makundi hayo kutokana na kutowajua vizuri wapinzani waliopangiwa nao.
” Tumeyapokea makundi hayo yote na kuichukua kama fursa ya kuendelea kujifunza zaidi Kwa muda tulionao kwani bado hatujui chochote kuhusiana na wapinzani wetu mpaka pale mashindano yatakapo Anza” alisema Shime.
Alisema licha ya kuwa wapo kwenye mtego mkubwa wa kutowajua kabisa wapinzani wao bado wanaendelea kujifunza yale yote waliyoyakusudia ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuweka heshima kwenye Taifa kwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote.
Aidha kocha Shime alisema mashindano hayo yamekuwa ni muhimu na faida kwa upande wa mwendelezo wa vipaji vya mabinti hao hususani wale watakao kidhi kucheza mashindano ya kufuzu World Cup kwa timu ya Taifa ya Wanawake U17, ambapo kocha Shime ametafsiri mechi hizo kuwa ni kipimo sahihi kwa wachezaji.