Issa Bukuku Aibariki Kozi ya Ukocha CAF Diploma D

Kozi ya ukocha ya CAF Diploma D inayojumuisha washiriki 52 imefunguliwa ramsi na kubarikiwa na mwenyekiti wa kamati ya ufundi ambaye pia ni mjumbe wa kamati tendaji TFF Issa Mrisho Bukuku Januari 28, 2022.

Kozi hiyo ya ukocha inayoendelea Makao Makuu ya TFF karume itaendeshwa kwa takribani  muda wa siku 10, huku mkurugenzi wa ufundi TFF Oscar Mirambo akiwa ndio mkufunzi mkuu wa kozi akisaidiana na wakufunzi wengine.

Mgeni rasmi wa kozi hiyo Issa Bukuku alisema kuwa hapo awali kamati ya ufundi ilikuwa ikipitia katika nyakati ngumu tofauti tofauti, kitu ambacho kwa kipindi hiki wamekuwa wakikifanyia kazi ili kutatua changamoto zote hizo katika kila maeneo yanayohusu mpira wa miguu nchini.

Eidha aliwataka washiriki hao kwenda kuwahamasisha wengine wengi zaidi hasa wanawake ambao bado bado wameonekana kujitokeza kwa uchache kwenye mafunzoya aina hiyo kwa lengo la kufikia ndoto zinazoendana na maono ya TFF ili kupata walimu wengi zaidi katika kila maeneo hasa kwa kipindi hiki ambacho TFF inaamini katika kuwekeza ziadi katika mpira wa vijana.

Kwa upande wa mkufunzi wa kozi hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi TFF Oscar Mirambo aliweka wazi lengo la TFF ni kukuza mpira wa vijana hapa nchini ndio mana imekuwa ikiendesha kozi mbalimbali za kuwajengea makocha wote uweledi wa juu zaidi wa mpira kulingana na wakati husika.

“Tunataka kuona ni namna gani tunaweza kupata matokeo ya hayo tunayowapatia kwa kipindi chote cha kozi, hivyo hatupo hapa kwaajili ya kuwapa vyeti bali ni kupata walimu wenye weledi wa mpiara ambao wanaweza kuzalishia Taifa wachezaji ambao ni bora zaidi”. Kauli ya Oscar Mirambo.

TFF imekuwa ikiandaa na kuendesha kozi za aina hiyo mara kwa mara lengo likiwa pia ni kuzalisha makocha wazawa wenye kuishi mpira wa miguu kwa falsafa inayofanana ili wote kwa pamoja kwenda kufundisha wachezaji watakao fanya vizuri katika kila mashindano ya kimataifa na yale ya vilabu.