Muamuzi wa Tanzania Jonesia Rukyaa ameingia kwenye rekodi ya kuwa Muamuzi wa kwanza wa Kike kuchezesha katika mashindano ya Afcon ya Wanaume baada ya kuchezesha mchezo uliochezwa Jumapili Aprili 21,2019 Chamazi ukiikutanisha Cameroon dhidi ya Senegal Afcon U17.
Rukyaa anayetajwa kuwa Muamuzi Bora wa Kike Afrika Mashariki alikua muamuzi wa katikati kwenye mchezo huo wa Kundi B Afcon U17 uliomalizika kwa timu hizo kutokufungana.
Itakumbukwa Rukyaa mwaka 2018 amechezeaha kwenye Fainali za Afrika za Wanawake AWCON zilizofanyika nchini Ghana.
Msimu uliopita 2017/2018 Ligi Kuu Tanzania Bara alichaguliwa kuwa Muamuzi Bora wa Ligi kwenye Tuzo za mwisho wa msimu.