Mwamuzi Jonesia Rukyaa kutoka Kagera atachezesha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania utakaowakutanisha Watani Simba na Young Africans utakaochezwa Jumamosi Januari 4 Uwanja wa Taifa.

Rukyaa atasaidiwa na Sudi Lilla na Hamis Chang’walu wote kutoka Dar es Salaam.

Mwamuzi wa akiba atakua Elly Sasii wa Dar es Salaam,Mtathmini Waamuzi Sudi Abdi wa Arusha na Kamishna wa mchezo Khalid Bitebo kutoka Mwanza.

Mchezo unatarajia kuanza saa 11 jioni.