Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana jana Jumapili Machi 10,2019 na kupitia mashauri mbalimbali yaliyofikishwa kwenye Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Wakili Kiomoni Kibamba.
KUSIKILIZA MASHAURI:
KESI NAMBA 01: SHAURI LA ABDALLAH SHAIBU (MCHEZAJI WA YANGA SC)
Mchezaji Abdallaha Shaibu amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa February 03 2019 kati ya timu yake na Coastal Union Fc alimpiga kiwiko mchezaji wa timu pinzani.
UTETEZI WA MLALAMIKIWA:
Mlalamikiwa(Shaibu) alikiri kupiga kiwiko wakati wa mchezo baada ya kuonyeshwa video ya tukio tajwa,Shaibu alijitetea kuwa hakuwa na dhamira ya kumpiga mchezaji wa timu pinzani, alikuwa anajaribu kumzuia asipite baada ya kuona amepiga pasi fupi kwa mchezaji mwenzake.
MAAMUZI:
Kamati imemtia hatiani Abdallah Shaibu kwa kosa la kumpiga kiwiko  mchezaji wa timu pinzani
Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.
Haki ya kukata rufaa iko wazi
KESI NAMBA 02: JUMA NYANGI (MCHEZAJI WA ALLIANCE FC)
Mchezaji Juma Nyangi amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Machi 02 2019 kati ya timu yake ya Alliance FC na Yanga SC alimfanyia kitendo cha udharirishaji mchezaji wa timu pinzani Gadiel Michael
UTETEZI WA MLALAMIKIWA:
Mlalamikiwa alikiri kosa na kuomba msamaha.
MAAMUZI:
Kamati imemtia hatiani Juma Nyangi kwa kosa la udharirishaji wa mchezaji wa timu pinzani
Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana na faini ya Tsh 2,000,000/= kwa mujibu wa kifungu cha 37(23) cha Kanuni za Ligi Kuu TFF.
Haki ya kukata rufaa iko wazi, adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.
KESI NAMBA 03: BENEDICT MLEKWA TINOCO (MCHEZAJI WA TIMU MTIBWA SUGAR FC)
Benedict Mlekwa Tinoco amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Februari 14 2019 kati ya timu yake ya Mtibwa Sugar na Biashara United Fc alimkanyaga kwa makusudi mchezaji wa timu pinzani aliyekuwa ameanguka baada ya kuchezewa rafu
UTETEZI WA MLALAMIKIWA:
Mlalamikiwa aliwakilishwa na kiongozi wa Timu yake, Ndg. Swabura Abubakar, mwakilishi wa mlalamikiwa alikiri kosa na kuomba msamaha.
MAAMUZI:
Kamati imemtia hatiani Benedict Mlekwa Tinoco kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa timu pinzani aliyekuwa ameanguka baada ya kuchezewa rafu
Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.
Haki ya kukata rufaa iko wazi
KESI NAMBA 04: SAMWEL PETER ( DAKTARI WA TIMU )
Ndg. Samwel Peter amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Februari 02 2019 kati ya timu yake na Rhino Rangers alifanya vitendo vya utovu wa nidhamu
UTETEZI WA MLALAMIKIWA:
Mlalamikiwa hakuwepo bila taarifa.
MAAMUZI:
Kamati imemtia hatiani Samwel Peter kwa kosa la kufanya vitendo  vya utovu wa nidhamu.
Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na mpira wa miguu kwa muda wa miezi mitatu na faini ya Tsh laki tano (500,000/=) kwa mujibu wa kanuni ya 41(7) kanuni za Ligi Daraja la Kwanza.
Haki ya kukata rufaa iko wazi, adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.
KESI NAMBA 05: MFAUME ALLY (KOCHA WA MAKIPA WA ARUSHA UNITED SC)
Ndg. Mfaume Ally amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Februari 02 2019 kati ya timu yake na Rhino Rangers alifanya vitendo vya utovu wa nidhamu
UTETEZI WA MLALAMIKIWA:
Mlalamikiwa hakuwepo bila taarifa.
MAAMUZI:
Kamati imemtia hatiani Mfaume Ally kwa kosa la kufanya vitendo  vya utovu wa nidhamu.
Kamati imempa adhabu ya kufungiwa michezo mitatu (3) na faini ya Tsh laki tano (300,000/=) kwa mujibu wa kanuni ya 40(1) kanuni za Ligi Daraja la Kwanza.
Haki ya kukata rufaa iko wazi, adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.
KESI NAMBA 06: LAURENT KIMARO (DAKTARI WA TIMU YA BIASHARA UNITED )
Ndg. Laurent Kimaro amelalamikiwa mbele ya kamati ya nidhamu kuwa Janaruari 25 2019 alitolewa kwenye benchi kwa kosa la kupinga maamuzi ya mwamuzi kati ya timu yake na Azam Fc.
UTETEZI WA MLALAMIKIWA:
Mlalamikiwa alituma utetezi wa maandishi na kukana kufanyika kwa kitendo hicho
MAAMUZI:
Kosa limeshindwa kuthibitishwa kwa upande wa mlalamikaji, hivyo basi kamati imetupilia mbali malalamiko haya.
KESI NAMBA 07: JOHN MCHEMBA (MENEJA WA TIMU YA TRANSITI CAMP )
Ndg. JOHN MCHEMBA amelalamikiwa Kamati ya Nidhamu kuwa tarehe 10/11/2018 katika mechi namba 31, kundi B dhidi ya Green Warriors iliyofanyika Azam Complex alianzisha vurugu na kusababisha mchezo kusimamishwa. Baadae alipelekwa jukwaa kuu lakini aliendelea na vurugu hizo.
MLALAMIKIWA:
Hakuwepo bila taarifa.
MAAMUZI:
Kamati baada ya kupitia ripoti zote, imetoa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2)ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini  ilipwe ndani ya siku 30.
KESI NAMBA 08: NELSON WILLIAM  (MENEJA WA TIMU YA POLISI TANZANIA )
Ndg. NELSON WILLIAM amelalamikiwa Kamati ya Nidhamu kuwa tarehe 19/01/2019 katika mechi namba 63, kati ya timu yake na Boma Fc alipigana na washabiki.
MLALAMIKIWA:
Hakuwepo bila taarifa.
MAAMUZI:
Kamati imemtia hatiani Ndg. Nelson William kwa kosa la kupigana na washabiki.
Kamati imetoa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na mpira wa miguu kwa muda wa miezi sita na faini ya Tsh laki nne (400,000/=) kwa mujibu wa kifungu cha 41(2) cha kanuni za ligi daraja la kwanza.
Vile vile kamati imetoa adhabu kwa timu ( Polisi Tanzania ) faini ya Tsh laki tano ( 500,000/=) kwa mujibu wa kanuni ya 15(2) kanuni za nidhamu za TFF,kwa kosa la kuendela kumtumia kiongozi ambaye amefungiwa kujihusisha na mpira wa miguu.
Kamati imeagiza bodi ya uendeshaji wa ligi, kuwa kama meneja tajwa hapo juu ataendelea kutumika basi timu ifutiwe matokeo kwa kila mchezo watakaomtumia, adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 12(e) ya kanuni za nidhamu TFF.
KESI NAMBA 09: GREEN PAUL  (MCHEZAJI WA TIMU YA POLISI TANZANIA )
GREEN PAUL amelalamikiwa Kamati ya Nidhamu kuwa tarehe 19/01/2019 katika mechi namba 63, kati ya timu yake na Boma Fc alimpiga mwamuzi msaidizi.
MLALAMIKIWA:
Hakuwepo bila taarifa.
MAAMUZI:
Kamati haikujiridhisha na utetezi wa mlalamikaji ivyo basi imetoa onyo kwa malalamikiwa kwa mujibu wa kifungu cha kanuni za nidhamu za TFF.
KESI NAMBA 10: MFUNGO BITA (MENEJA WA KASULU RED STAR FC  )
Ndg. MFUNGO BITA amelalamikiwa Kamati ya Nidhamu kuwa tarehe 17/11/2018 alifanya vitendo vya utovu mkubwa wa nidhamu  kwenye mechi dhidi ya bulyanhulu Fc na  kasulu red star.
MLALAMIKIWA:
Hakuwepo bila taarifa.
MAAMUZI:
Kamati imemtia hatiani Mfungo Bita kwa kosa la kufanya vitendo  vya utovu wa nidhamu.
Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutojihusisha na mpira wa miguu kwa muda wa miezi mitatu na faini ya Tsh laki tano (500,000/=) kwa mujibu wa kanuni ya 41(7) kanuni za Ligi Daraja la Pili.
Haki ya kukata rufaa iko wazi, adhabu zote zinakwenda kwa pamoja