Kikosi cha Timu ya Taifa (Twiga Stars) Kambini Kwa Michezo Miwili ya Kirafiki

Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Taifa (Twiga Stars) kimeingia kambini Mei 24, 2024 kujiandaa na mechi za kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA inayo tarajiwa kucheza mwishoni mwa mwezi huu.

Twiga Stars ikiongozwa na kocha mkuu Bakari Shime inatarajia kucheza michezo miwili na timu ya Taifa ya Mali na Sudan Kusini.

Wachezaji walioitwa kambini ni; Najiat Abbas, Asha Mrisho, Lidya Maximilian, Krista Bahera, Julietha Singano, Enekia Kasonga, Vaileth Nicholaus, Suzan Adam, Ester Maseke, Diana Lucas,Jamila Rajabu, Winfrida Gerald, Aisha Mashaka, Janet Pangamwene Joyce Lema na Opa Clement.

Wengine ni; Stumai Abdallah, Aisha Mnuka,Clara Luvanga, Aliya Fikiri, Asha Omary na Maimuna Kaimu.

Tanzania (Twiga Stars) itacheza mechi ya kwanza dhidi ya Mali mwezi Mei 29, 2024, kabla ya kukutana na Sudani Kusini Mei 31, 2024. Wakati michezo mingine ya kirafiki itazikutanisha Seychelles na Sudani Kusini Mei 31, 2024 na Mei 31, 2023 timu ya Taifa ya Mali itacheza na Seychelles.