Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inakabiliwa na mchezo muhimu dhidi ya Uganda wa kufuzu kucheza Fainali za Afrika mwaka huu.

Huu ni mchezo ambao kama Taifa Stars itashinda inaweza kukata tiketi ya kucheza AFCON mwaka huu itakayofanyika nchini Misri.

Mchezo dhidi ya Uganda utachezwa Jumapili Machi 24,2019 saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike ametangaza kikosi kitakachopambana kuisaka tiketi hiyo kwenye Uwanja wa nyumbani.

Nahodha Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk ya Belgium ataongoza kikosi katika mchezo huo uliobeba imani ya Watanzania.

Kocha Amunike amesema Kikosi alichokitaja kimezingatia mambo mengi kuhakikisha Taifa Stars inapata ushindi.

Amewataka Watanzania kuiunga mkono Taifa Stars katika kuipeperusha bendera ya Tanzania.

Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), George Mango amesema kampuni hiyo imekuwa ikihakikisha kikosi hicho kinafanya maandalizi mazuri ili kufanya vema kwenye mchezo ujao na hatimaye iweze kuibuka na ushindi na kukata tiketi kucheza Afcon.

“Siku zote kinywaji cha Serengeti Premium Lager ni shabiki mkuu wa Taifa Stars na mdhamini mkuu pia. Katika mchezo huu tumejidhatiti kuhakikisha timu yetu inaibuka na ushindi ambao utakuwa fahari kwa Taifa letu na kwa kinywaji chetu cha Serengeti,” alisema Mango.

Mango aliwataka mashabiki wa soka nchini kufika kwa wingi siku ya mchezo huo ili kuwapa hamasa wachezaji kwaajili ya kuipa ushindi timu hiyo ya Taifa.

Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa:

1.Aishi Manula -Simba
2.Feisal Salum -Young Africans
3.Hassan Kessy-Nkana,Zambia
4.Yahya Zayd-Ismaily,Misri
5.Gadiel Michael-Young Africans
6.Himid Mao-Petrojet,Misri
7.Mudathir Yahya-Azam FC
8.Shaaban Chilunda-Tenerife,Hispania
9.Kelvin Yondan-Young Africans
10.Shiza Ramadhan-ENPPI,Misri
11.Simon Msuva-El Jadida,Morocco
12.Rashid Mandawa-BDF,Botswana
13.Jonas Mkude-Simba
14.Mbwana Samatta-KRC Genk,Belgium
15.Thomas Ulimwengu-JS Saoura,Algeria
16.Mechata Mnata-Mbao FC
17.Aron Kalambo-Tz Prisons
18.Suleiman Salula-Malindi FC,Zanzibar
19.Vicent Phillipo-Mbao
20.Ally Mtoni-Lipuli
21.Andrew Vicent-Young Africans
22.Kennedy Wilson-Singida United
23.Aggrey Morris-Azam FC
24.John Bocco-Simba
25.Farid Mussa-Tenerife,Hispania