Kim Poulsen Atangaza Kikosi Kipya cha Taifa Stars

Kocha mkuu wa timu ya Taifa “Taifa Stars” Kim Poulsen leo hii  Februari 26, 2021 amekitangaza kikosi kitakachoingia kambini tayari kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki huko Kenya pamoja na michezo ya kufuzu AFCON dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.

Ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya mkutano na waandishi wa habari tangu kuteuliwa kwake kukinoa kikosi hiko, kocha huyo amesema kwamba amefurahi sana kurudi tena Tanzania na kupata nafasi hiyo kwa mara nyingine, hivyo basi amejipanga kuhakikisha kwamba timu ya Taifa inafanya vizuri na inaendelea kuimarika.

Kocha Poulsen amesema kwamba vigezo alivovitumia katika kukichagua kikosi hiko ni pamoja na mtazamo chanya alionao mchezaji lakini kubwa zaidi ni ule ufahari ambao mchezaji anauona au kuwa nao kwa kuichezea nchi yake. Pia hakuacha kusisitiza juu ya kigezo cha kujituma na kujitoa kwa hali zote ili kuhakikisha timu inapata mafanikio.

Kikosi hiko kimejumuisha wachezaji wafuatao:Aishi Manula (GK) Simba, Metacha Mnata(Gk) Young Africans, Juma Kaseja (Gk) KMC FC,Shomari Kapombe (RF) Simba, Hassan Kessy (RF) Mtibwa sugar, Israel Mwenda (RF) KMC FC, Erasto Nyoni (CD) Simba , Dickson Job (CD) Young Africans, Bakari Nyondo Mwamnyeto (CD) Young Africans,Kelvin Yondan (CD) Polisi Tanzania, Carlos Protas (CD) Namungo FC, Kennedy Juma (CD) Simba, Laurent Alfred Laurent (CD) Azam FC, Mohammed Hussein (LF) Simba , Nickson Kibabage (LF) Youssoufia FC – Morocco, David Bryson(LF) KMC FC, Y assin Mustapha (LF) Young Africans, Edward Manyama (LF) Ruvu Shooting, Simon Msuva (RM) Wydad  AC – Morocco, Hassan Dilunga Ayoub Lyanga(RM) Azam FC, Novatus Disma s Miroshi(CM) Macab  Tel Aviv-Israel, (R/LM) Simba, Mzamiru Yassin (CM) Simba , Jonas Mkude(CM) Simba, Saidi Juma Ndemla (CM) Simba, Feisal Salum (CM) Young Africans, Hamid Mao (CM)  El Entag SC Egypt, Ally Msengi (CM) Stellenbosch FC-South Africa, Baraka Majogoro(CM) Mtibwa Sugar, Salum Abubakar (CM) Azam FC, Farrid Mussa (LM) Young Africans, Iddy Suleiman Nado (LM) Azam FC, Mbwana Samatta(FW) Fenerbahce FC – Turkey, Thomas Ulimwengu (FW) TP Mazembe – DR Congo, John Bocco(FW) Simba, Yohana Mkomola (FW) Inhulets Petrove – Ukraine, Shaaban Iddi Chilunda(FW) Moghreb FC- Morocco, Ditram Nchimbi (FW) Young Africans, Deuis Kaseke (FW) Young Africans, Abdul Hamis Suleiman (FW) Costal Union, Kelvin Pius John (FW) Brooke House College –UK, Nassor Saadun Hamoud (FW) MFK-Czech , Meshack Abraham Mwamita,(FW) Gwambina.

Mbali na hayo kocha huyo amesema kwamba hatafanya mabadiliko yoyote katika benchi la ufundi kwani hajaona sababu ya kufanya hivyo kwa sasa.