Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Queens” imepangwa katika Kundi A kwenye ratiba ya mashindano ya Wanawake ya CECAFA iliyotolewa leo.
Katika kundi A mbali ya Tanzania Bara timu nyingine zilizopo ni Zanzibar,Burundi na Sudan Kusini.
Kundi B lina timu za Ethiopia,Kenya,Uganda na Djibouti.
Mashindano yanatarajia kuanza Novemba 14,2019 na kufikia tamati Novemba 24,2019,Azam Complex,Chamazi