Timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ leo itafanya mazoezi ya kwanza tokea imewasili jijini Kampala ikiwa ni muendelezo wa maandalizi yake kwa mashindano ya Cecafa Chalenji yanayoanza kesho Disemba 7.
Mazoezi hayo ya Stars yatafanyika saa 10 Jioni katika viwanja vya Kawempe ambavyo viko umbali wa Kilomita 5 kutoka katika hoteli ambayo imefikia ya Sojovaro.
Kwa mujibu wa kocha Mkuu Juma Mgunda, mazoezi ya leo yatakuwa ni mepesi ya kuondoa uchovu wa safari sambamba na mbinu kiasi.
“Vijana wako vizuri na tunashukuru wote ni wazima tangu tulipowasili jana hadi leo hii,Molali na hamasa yao iko juu na kikubwa tunawaomba Watanzania waendelee kutupa sapoti na kutuombea, ” amesema Mgunda.
Kilimanjaro Stars itaanza kibarua cha kuusaka Ubingwa Jumapili dhidi ya Kenya