Kocha Mkuu Etiene Ndayilagije Aanika Kikosi Kitakachovaana na Burundi Oktoba
Kikosi kipya cha timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kimetangazwa leo Oktoba 2, 2020 mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Akitangaza kikosi hicho kinachoongozwa na kocha Mkuu Etiene Ndailagije Ofisa habari wa TFF Clifford Mario Ndimbo amesema kuwa kikosi hicho kinatarajia kukutana na timu ya Taifa ya Burundi (“ntamba m’rugamba”) katika mechi ya kirafiki siku ya Jumapili Oktoba 11, 2020 katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaaam.
Mechi hiyo ya kirafiki kati wa wenyeji Tanzania (Taifa Stars) na Burundi ni mchezo unaotambulika na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA na unachezwa kwa mujibu wa ratiba ya shirikisho hilo.
Baadhi ya wachezaji wanaounda Kikosi hiko ni pamoja na: David Mapigano (Azam Fc), Aisha Manula (Simba Sc), David Kisu (Azam Fc), Shomari Kapombe (Simba Sc), Israel Mwenda (KMC Fc), Mohamed Hussein (Simba Sc), Brayson David (KMC Fc),Bakari Mwamnyeto (Young Africans), Abdallah Sebo (Azam Fc), Dickson Job (Mtibwa Sugar), Iddi Mob (polisi Tanzania), Jonas Mkude (Simba Sc), Himid Mao (ENPPI Sc-Misri), Simon Msuva (Diffa EL ladid-Morocco), Ditram Nchimbi (Young Africans), Feisal Salum (Young Africans), Ally Msengi (Stellenbosch Fc-Afrika kusini), Mbwana Samatta (Fenerbache Fc- Uturuki), John Bocco (Simba Sc), Mzamiru Yassin (Simba Sc), Iddy Nado (Azam Fc), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe-DRC Congo), Nickson Kibabage (Diffa El Tadidi-Morroco), Said Hamis (Simba Sc), Salum Abubakar (Azam Fc).
Kikosi hicho chenye jumla ya wachezaji 25 kinatarajiwa kuingia kambini mnamo tarehe 05 Oktoba, 2020.