Kocha Shime Aridhishwa na Uwezo wa Nyota Wake
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” Bakari Shime ameweka wazi kirudhishwa na Uwezo walioonyesha nyota wake kwenye mechi mbili za kimataifa za kirafiki zioizochezwa mwishoni mwa mwezi Mei hapa nyumbani Tanzania.
Kocha Shime alieleza hayo mara baada ya kumalizika Kwa mechi ya pili dhidi ya Mali iliyochezwa Mei 31, 2024 uwanja wa Azam Complex Chamazi na kumalizika Kwa matokeo ya sare ya kifungana magoli 2-2.
Baada ya mchezo huo Shime aliwapongeza wachezaji wake Kwa ubora mkubwa waliokuwa nao hasa katika kumiliki mpira Kwa muda mrefu huku wakipelwka mashambulizi yaliyo pelekea kuongeza presha kubwa Kwa wapinzani wao.
Aidha alisema licha ya kupata matokeo ya sare, kwake mechi hiyo imekuwa ni kipimo sahihi hasa Kwa kujiandaa na mashindano ya WAFCON ambayo pia hata timu ya Taifa ya Mali pia itashiriki michuano hiyo hapo baadae.
“Tumeweza kuona mapungufu na ubora wetu, lakini pia nimeridhishwa na kiwango Cha wachezaji Kwa ujumla. Kupitia mechi hizi tumepata muelekeo wa kuangali wapi hasa tutaanzia Kwa maandalizi ya mashindano yaliyo mbele yetu” alisema Shime.
Mbali na hayo pia kocha aligusia swala la nyota wa Tanzania wanaokipiga nchi za nje kwamba ni sehemu ya mipango ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhakikisha wanakuwa na sehemu ya wachezaji wengine pia wa timu ya Taifa wanao cheza nje ya Tanzania.
Hata hivyo Twiga Stars ilicheza mechi mbili za kirafiki wakianza na timu ya Taifa ya Sudani Kusini Mei 29, 2024 mchezo uliomalizika Kwa Tanzania kupata ushindi wa magoli 3-0 kabla ya kumalizana na Mali.