Kocha wa zamani wa timu ya Taifa Taifa Stars Rudi Gutendorf amefariki leo akiwa na miaka 93.

Katika uhai wake,Gutendorf aliwahi kukinoa kikosi cha Taifa Stars ambapo moja ya mafanikio ni kukiwezesha kikosi hicho kufika hatua ya Fainali Kombe la Challenge mwaka 1981.

Gutendorf anashikilia rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kufundisha timu 55 katika mataifa 32 yaliyopo kwenye mabara 5.

Mara ya mwisho kufundisha ilikua mwaka 2003.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,Amina