Kozi ya CAF C Diploma yaendelea TFF

Moduli ya tatu ya kozi ya ualimu wa mpira wa miguu CAF C diploma inaendelea makao makuu ya TFF Ilala, Dar es salaam ikijumuisha washiriki 45 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Kozi hiyo ya nadharia na vitendo chini ya mkufunzi Oscar Mirambo itatamatishwa mapema mwezi disemba baada ya washiriki wote kufanya mitihani rasmi na watakaofaulu ndio watakaotunukiwa vyeti.

Akizungumzia maendeleo ya kozi hiyo Mratibu wa Kozi Raymond Gweba alisema, kozi imekwenda vizuri na amefurahishwa na utayari waliouonesha washiriki wa kutaka kujifunza, hivyo anaamini watakwenda kutumia ujuzi walioupata kukuza soka la Tanzania.

Washiriki wa mafunzo hayo ni; Aloyce Mathew, Mohammedi Abdallah, Isaya Mganda, Abdallah Mbonde, Frank Faraja,Joshua Charles, Armstrong Clement, Joseph Christian, Monja Liseki, Kisa .L. Peter, Mussa Namkoveka, Hilali Uwesu, Shabani Bakari,Ali Khamis, Maimuna Hamu, Adelard Mishinga, Khalifa Omary,Ramadhani Juma, Yahya Salum na Omari Matwiko.

Wengine; Henry Hezron, Juma Mohammed, Sylvester Aldor, Haji Ali, Matoka Ahmad, Kulinganila Kulinganula, Newland Kisyeri, Athumani Athumani, Sitta Shija, Katungunya Katungunya, Dickens Edgar, Said Abdallah, Titho Kithojo, Rich Oscar, Hassan Juma, Joseda Patrick, Henry Shindika, Amri Kiemba, Victor Hussein, James Haule, Athuman Idd, Yusuph Mohamed na James Mhagama.