Kozi ya Ukocha Diploma B CAF inatarajia kufanyika Dar es salaam Machi 4-Aprili 10,2020.

Ada ya ushiriki ni shilingi 800,000.

Anayehitaji kushiriki katika Kozi hiyo awasiliane na Mkurugenzi wa Ufundi TFF Oscar Mirambo mapema.

Tayari kumefanyika Kozi mbalimbali za Diploma C ya Ukocha na sasa inakwenda kufanyika Diploma B ikiwa chini ya mkufunzi wa CAF.