KOZI YA GRASSROOT YAENDELEA KUPAMBA MOTO

Mafunzo ya kozi ya Grassroot inayotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kushirikiana na FIFA yamendelea hii leo May 5, 2021 katika uwanja wa Karume, Dar es salaam.

Kozi hiyo yenye lengo la kutoa elimu kwa washiriki ni namna gani ya kukuza na kuendeleza vipaji vya kucheza mpira wa miguu kwa watoto wadogo katika ngazi ya awali kabisa ilianza rasmi May 03, 2021 huku ikijumuisha washiriki 52 na inatarajiwa kumalizika siku ya Ijumaa ya May 07, 2021.

Mkufunzi wa kozi hiyo ya Grassroot , Raymond Gweba amewapongeza sana washiriki wote waliyo jitokeza hususani walimu kutoka katika vituo mbalimbali vya kukuzia mpira kwa vijana wenye umri mdogo lakini pia hakusita kusifia mwitikio mkubwa kwa washiriki katika kujifunza na kuuliza maswali pia.

Mafunzo haya yatatolewa kwa siku 5 kwanzia May 03, 2021 mpaka May 07, 2021 na yanamjumuisho wa washiriki 52.