Kozi ya Maboresho (Refresher Course) ya CAF A diploma yahitimishwa Mnyanjani,Tanga
Kozi ya Maboresho (refresher course) ngazi ya CAF A diploma imehitimishwa rasmi Leo na Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia katika kituo cha ufundi cha TFF kilichopo Mnyanjani, Tanga.
Kozi hiyo iliyojumuisha waalimu wa mpira wa miguu 26 ambao tayari wana vyeti vya CAF A diploma ilikuwa na lengo la kuwakumbusha majukumu yao ya kiuterndaji na kuwaongezea ujuzi utakaowasidia kuendana na mabadiliko ya mfumo wa soka la kisasa.
Akihitimisha kozi hiyo Rais wa TFF walace Karia alisema, ulimwengu wa mpira wa miguu umebadilika sana ukilinganisha na zamani, hivyo na Tanzania lazima ibadilike ili iweze kufikia maendeleo makubwa.
” Ukichagua kuwa mwalimu wa mpira wa miguu basi uwe tayari kujifunza na kuangalia wenzako waliofanikiwa wanafanya nini, hivyo niwapongeze waalimu wote mlioshiriki katika kozi hii na TFF kupitia idara yake ya ufundi itaendelea kutoa kozi mbalimbali za ukocha na nyinginezo ili lengo la kuifanya Tanzania kwa kitovu cha michezo liweze kufikiwa”.
Washiriki wa kozi ni Rogasian Kaijage, Dr. Msindo Msolwa, Ally Mtumwa, Mohammed Rishard, Jamhuri Kihweru, Fred Felix, Juma Mwambusi, Nasra Mohammed, Hamim Mawazo, Salum Shaban Mayanga, Charles Boniface Mkwasa, Hemed Morroco, Malale Hamsini, Emmanuel Raymond Massawe.
Wengine ni Mohamed Tadjin, Dismas Godon Haonga, Juma Ramadhan Mgunda, Meck Maxime Kiaga, Ali Vuai Shein, wane Nelson Mkisi, Salum Ali Haji, Abdallah Mohamed Juma, Abdulmutik Haji Ali, Maka Andrew Mwalwisi, Hababuu Ali Omary na Sebastian Leonard Nkoma.
Kozi ya maboresho ya CAF A diploma iliendeshwa chini ya mkufunzi Oscar Mirambo na Hanour Janza ikifanyika kwa muda wa siku 6 na kuhitimishwa kwa washiriki wote kutunukiwa vyeti.