Ligi Kuu Bara Ni Zaidi ya Vita

Michezo kadhaa ilipingwa wikiendi hii kati ya tarehe 18 na 19 Februari, 2023 ambapo timu zote tatu zilizokuwa nyumbani zilifanikiwa kuibuka na ushindi Idadi sawa ya magoli baada ya timu hizo kupachika bao moja moja.

Michezo hiyo iliyopigwa kwenye Viwanja vitatu tofauti; timu ya Kagera Sugar ili ichapa  Namungo bao moja ilipoialika nyumbani (Katiba), Coastal Union iliwalaza Mbeya City Kwa bao moja pia ikiwa Mkwakwani Tanga huku Polisi Tanzania nao wakifufua matumaini mara baada ya kuwachezesha kwata maafande wenzao Tanzania Prisons kwa bao moja.

Mchezo wa Polisi Tanzania na ule Wa tarehe 18 uliowakutanisha Mbeya City na Coastal Union ndiyo ilikuwa ya vuta ni kuvute kufuatia ushindani mkali wa nafasi  za nani ashuke na nani acheze mechi za mtoano.

Ushindi wa Coastal Union ulifanya timu hiyo inayosuasua kwa sasa kupanda nafasi moja ikifikisha alama 22 sawa na Prisons, wakati Polisi Tanzania nao walifanikiwa kusogea kwenye nafasi ya 15 baada ya kufikisha alama 19, wakiwashusha Ruvushooting Wenye alama 17; huku Kagera Sugar wao wakijiongezea alama na kufikisha 29 wakiwa nafasi ya 6, Namungo  ikiwa  ya 7 na Mtibwa Sugar wao wakishika nafasi ya 8. Timu zote tatu zimefungana kwa alama huku zikitofautishwa na Idadi ya  magoli ya kufunga na kufungwa.

Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania Mohammed Abbas baada ya mchezo dhidi ya maafande wenzao Tanzania Prisons alisema kuwa kikosi hicho Kwa sasa kinazidi kuimarika siku Hadi siku maana ushindi walioupata unaifanya timu kuendelea kutokupoteza mchezo Kwa mechi sita mfululizo baada ya kutoka sare kwenye mechi nne na kushinda miwili. Aliongeza kuwa wanazidi kujipabga zaidi ili waweze kupata matokeo mazuri zaidi kwani safu ya ulinzi imekamilika kilichosalia ni umaliziaji wa nafasi za magoli wanazozipata tu.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Tanzania Prisons, Shabani Mtupa, alisema kuwa wachezaji wake wamepambana kutafuta ushindi lakini kukosekana Kwa umakini Wa kutosha kwenye umaliziaji wa nafasi wanazozipata ndiyo sababu ya kupoteza mchezo huo. Kocha huyo alielezea kwenda kuyafanyia kazi makosa hayo ili waweze fanya vizuri kwenye michezo inayofuata ya Ligi ya NBC.

Ligi hiyo ya NBC inazidi kuwa ngumu kwani mpaka mzunguko Wa 22/23 bado Kuna vita kali ya nani anachukua ubingwa, nani anabaki kwenye nafasi ya pili huku vita nyingine ikiwa nani anaingia kwenye nne Bora achilia mbali vita ya wanaogombea kutoshuka daraja wakati wengine pia wanaogombea walau kucheza mechi za mtoano.