Ligi Kuu ya NBC Hakuna Kulala

Mechi kadhaa za Ligu Kuu Bara ziliendelea Novemba 17, 2022 ambapo kwa mara ya kwanza  timu ya Young Africans ilifanikiwa kuiadhibu Singida Big Stars (SBS) kwa jumala ya mbao 4-1 kwenye mchezo uliopigwa majira ya saa 1:00 usiku kwa Mkapa.

Young Africans ilikuwa mwenyeji dhidi ya SBS ambao walishindwa kuonesha makeke katika mchezo huo baada ya kocha Nasreddine Nabi kuwapangia kikosi kilichomaliza msimu uliopita pasipo kupoteza mechi. Hali ya mchezo huo ilikuwa ni nzuri kwa wenyeji huku wageni SBS wakionekana kutoiumudu mechi hiyo kutokana na kiwango bora walichokionesha Young Africans kwa dakika zote 90.

Magoli matatu ya Fiston Mayele na moja la Kibwana Shomari yalitosha kuingamiza SBS kwenye mchezo huo licha ya mshambuliaji na mfungaji bora wa misimu miwili akiwa Simba, Meddie Kagere kuwaandikia waajiri wake wapya bao la kufutia machozi (65) bado halikutosha timu ya walima alizeti hao kurejea na kuukamata mchezo huo.

Mbali na mchezo huo wa Young Africans na SBS,  michezo mingine iliyopigwa siku hiyo ilikuwa ni ule wa Mbeya City dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilimalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu baada ya kufungana mabao 2-2. Mabao ya Kagera yalifungwa na AnuaryJabir  na Mbaraka Yusuph wakati upande wa Mbeya City yalipachikwa na Tariqy Seif na Hassan Mahamud.Katika mchezo huo Mbeya City walipata penati ambayo haikuweza kuzaa goli baada ya nyota na kinara wa mabao wa timu hiyo Sixtus Sabilo kushindwa kuukwamisha kimiani mpira na hivyo kulifanya lango la Kagera Sugar kubakia salama kwa muda huo.

Mchezo wa mapema zaidi ulikuwa ule wa saa 08:00 kati ya Ihefu FC na Polisi Tanzania katika uwanja wa nyumbani wa Ihefu Mbalali.  Mchezo huo ulimalizika kwa Ihefu kupokea kipigo cha mabao 2-1 mabao ya Polisi yalifungwa na Vitalisy Mayanga dakika ya 51 na Samweli Ondit (78, OG) huku bao moja la Ihefu FC likifungwa na Andrew Simchimba mapema mnamo dakika ya 19 ya mchezo huo.

Wakati hakuna kulala ikitokea kwenye mnyukano wa alama, vita nyingine ni kwa wafungaji wanao wanaia ufungaji Bora msimu huu 2022/2023 Mpaka Novemba 17, 2022 mfugaji kinara alikuwa ni Sixtus Sabilo wa Mbeya City (7); huku Fiston Mayele, Moses Phiri, Reliant Lusajo na Idris Mbombo wa Azam wote wakifungana kwa kuwa na idadi ya  mabao 6.

Matokeo ya mchezo huo  yanaifanya Young Africans kurejea katika uskani wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara nyingine baada ya kufikisha alama 26 wakiondosha Azam FC waliokuwa wakiongoza kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.