Fainali za ligi kuu ya vijana U20 2021
Fainali za ligi ya vijana U20 2021 zimendelea June 15, 2021 kwa michezo miwili iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex , Dar es Salaam.

Tanzania Prison U20 ulishuka uwanjani dhidi ya Azam FC U20 mchezo uliokuwa na ushindani wa hali ya juu sana timu zote zilingia uwanjani zikisoma mchezo wa mwenzake mpaka dakika ya 17 hivi Azam FC U20 walipoamua kuongeza mashamulizi kwa wapinzani wao lakini haikuwafanya kupata goli mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika na matokeo ya 0-0.

Kipindi cha pili Azam FC walirudi kwa kasi kidogo kulinganisha na wapinzani wao licha ya kufanya mabadiliko mengi lakini haikusadia kubadilisha hali ya mchezo na kufanya kipindi cha pili pia kumalizika kwa matokeo ya 0-0.

Huku kocha wa timu ya Azam FC U20 , Vivier Bahati akiwapongeza wachezaji wake kwa kucheza mchezo mzuri lakini mawazo yao kwa sasa watangalia mchezo unaofata dhidi Young Africans U20 na wanamini watapita pia katika hatua hiyo kwani wanaifahamu vizuri timu hiyo kwa sababu walikuwa katika kundi moja huko awali.

Kwa upande wa mwalimu wa Tanzania Prisons U20 , Shabani Mtupa alianza kwa kuwapongeza vijana wake kwa kupambana licha ya kukosa nafasi ya kuendelea lakini hakusita kuwapongeza Azam FC U20 kwa kuonesha mchezo mzuri na kusema “ Mpango tuliopanga tucheze leo umefanikiwa kwa asilimia kubwa lakini katika eneo la ushambuliaji tu ndo tulikuwa na makosa lakini tumeyaona na tutayafanyia kazi huko mbeleni” alisema Mtupa.