Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajia kuendelea leo kwa mchezo mmoja kuchezwa Uwanja wa Uhuru.
Timu ya KMC watakuwa wenyeji wa timu ya Azam FC katika mchezo huo wa raundi ya Kwanza.
Mchezo huo utaanza saa 10 jioni.
Baada ya mchezo wa leo,mchezo mwingine wa VPL utachezwa Kesho Jumatano wakati Young Africans watakapowaalika Ruvu Shooting ya Pwani.
Pazia la msimu wa 2019/2020 limefunguliwa rasmi Jumamosi Agosti 23 kwa kuchezwa michezo mitano