Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) itachezwa katika vituo vinne katika Mikoa ya Tanzania Bara, ikianza Machi 27, 2019 na kumalizika April 11, 2019 katika hatua ya Makundi.
Timu mbili (2) za juu kutoka katika kila kundi zitafuzu kucheza hatua ya Nane (8) Bora katika kituo kimoja kitakachotangazwa na TFF.
Hatua ya nane Bora itakua na makundi mawili (2) yenye timu nne kwa kila kundi, ambapo timu mbili za juu zitafuzu hatua ya Nusu Fainali na hatimae Fainali.
Washindi watatu (3) watapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Pili msimu wa 2019/2020
Vituo vya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) 2018/2019 ni:
1. SIMIYU – Uwanja wa Halmashauri Bariadi
2. KATAVI – Uwanja wa Azimio Mpanda
3. SONGWE – Uwanja wa Vwawa Mbozi
4. DODOMA – Uwanja wa Mgambo Mpwapwa
KUNDI A – SIMIYU:
Bariadi United (Simiyu), Copco Veteran (Mwanza), Hawita (Mara), Mbuni FC (Arusha), Red Star (Manyara), Buyuni FC (Dar es salaam), Ujenzi FC (Shinyanga).
KUNDI B – KATAVI:
Mkurugenzi FC (Katavi), Mpui FC (Rukwa), Sabasaba FC (Tabora), Tallinega FC (Kigoma), Isanga Rangers (Mbeya), Masumbwe FC (Geita), Umoja Chandimu (Kagera).
KUNDI C – SONGWE:
Mpira Pesa FC (Songwe), Deportivo Mang’ula (Morogoro), Makete United (Njombe), Coastal Star (Pwani), Nzihi FC (Iringa), Top Boys (Ruvuma), DTB FC (Dar es salaam).
KUNDI D – DODOMA:
Mji Mpwapwa FC(Dodoma), Pan African (Dar es salaam), Stand Misuna (Singida), Majengo United (Tanga), New Generation (Kilimanjaro), Timberland FC (Lindi), Tandahimba FC (Mtwara).
Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.