LIGI KUU ya soka la ufukweni Tanzania Bara (BSL) inatarajia kuanza Februari 9,2019 mpaka April 14,2019.
Ligi hiyo itakua inachezwa kwenye Uwanja wa COCO BEACH uliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam kila Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 8 mchana mpaka 12 jioni.
Kuelekea kwenye Ligi hiyo,TFF imeanza kusajili vilabu vyenye sifa na vigezo ili kushiriki.
Fomu za usajili zinapatika katika ofisi za TFF Makao Makuu,Karume,Ilala Dar es Salaam kwa ada ya shilingi laki moja (100,000).
Kila timu itapatiwa mipira miwili ya soka la ufukweni kutoka TFF baada ya kukamilisha usajili na kulipa Ada ya usajili.