Ligi ya Vijana U20 kwa Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuanza Mei 4,2019.
Timu 20 za Ligi Kuu zinatarajia kuumana kumtafuta bingwa wake katika mtindo wa Nyumbani na Ugenini.
Ligi hiyo itashirikisha timu za Azam,Simba,Young Africans,Lipuli,Mtibwa,,Kagera Sugar,Prisons,Mbeya City,African Lyon,JKT Tanzania na Coastal Union.
Nyingine zitakazocheza Ligi hiyo ni Ndanda,Alliance,Mwadui,Stand United,Biashara,Ruvu Shooting,KMC,Mbao na Singida United.