Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Machi 3, 2020 ilipitia taarifa mbalimbali za mechi ya Ligi Kuu Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) zinazoendelea hivi sasa.

LIGI KUU

Mechi namba 247- Mtibwa Sugar FC 2 vs Ndanda FC 1

Timu ya Ndanda FC imetozwa faini ya Tsh 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi na kuliacha gari tupu likipita katika mlango rasmi katika mchezo tajwa uliofanyika Februari 29, 2020 uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.

Adhabu inatolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 14(43) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

LIGI DARAJA LA KWANZA

Mechi namba 94- Arusha FC 0 vs Gipco FC 2

Klabu ya Arusha FC imetozwa faini ya Tsh 500,000 (laki tano) kwa kosa la mashabiki wake kuingia uwanjani na kuanza kuwashambulia waamuzi na wachezaji wa timu pinzani na kusababisha mmoja wa waamuzi Abdalla Uako kuibiwa simu yake na mwingine kuumizwa mkono katika mchezo huo uliofanyika Februari 29, 2020 uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Endapo vitendo hivyo vitajirudia tena katika mchezo mwingine watakaocheza, Kamati haitasita kuchukua maamuzi makubwa zaidi ikiwemo kuwabadilishia uwanja wa nyumbani wa klabu yao (home ground) na kupangiwa uwanja mwingine.

Klabu itawajibika kulipa hasara aliyopata mwamuzi Abdallah Uako ya kupoteza simu.

LIGI DARAJA LA PILI

Mechi namba 42A- Rufiji FC 0 vs Mbuni FC 2

Mchezaji wa Mbuni FC (Kapteni) Geofrey Msemwa ametozwa faini ya Tsh 500,000 (laki tano) na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kutoa lugha chafu kwa waamuzi wakati wa ukaguzi na kukaidi kuomba radhi pale alipoelekezwa katika mchezo huo tajwa uliofanyika February 29, 2020 katika uwanja wa CCM Azimio Rufiji.

Adhabu kwa uzingativu wa kanuni ya 38(7) ya Ligi daraja la pili Kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Kocha wa timu ya Mbuni FC Leonard Budeba ametozwa faini ya Tsh 300,000 (laki tatu) na kufungiwa michezo mitatu (3) kwa kosa la kutoa lugha chafu na kusababisha kupewa kadi ya njano katika mchezo uliofanyika Februari 29, 2020 uwanja wa CCM Azimio Rufiji.

Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni ya 41 ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Makocha.

Klabu ya Mbuni FC imetozwa faini ya Tsh 200,000 (laki mbili) kwa kosa la viongozi wa timu hiyo waliovaa sare za jeshi kuwatishia watazamaji wa mchezo na hata mchezo ulipomalizika viongozi hao waliimba nyimbo za kukashifu katika mchezo tajwa uliofanyika Februari 29, 2020 uwanja wa CCM Azimio Rufiji.

Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Pili Kuhusu Udhibiti kwa Viongozi

Mchezaii wa timu ya Mbuni FC Sinai Sadik Siri aliyepewa kadi nyekundu katika mchezo huu tajwa ametozwa faini ya Tsh 300,000 (laki tatu) na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga mchezaji wa timu pinzani.

Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni ya 38 (3) ya Ligi Daraja la Pili Kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Mechi namba 32C – Bulyanhulu FC vs Milambo FC- \
Milambo FC imepewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu kwenye mchezo uliokuwa ufanyike Februari 28, 2020 katika uwanja wa Barick Gold Mine mkoani Shinyanga, baada ya timu ya Bulyanhulu FC ambayo ndio timu mwenyeji kushindwa kuleta gari la wagonjwa (Ambulance) uwanjani na kusababisha mchezo kuvunjwa na mwamuzi wa mchezo huo tajwa